Naomba kujua tofauti kati ya Kushinda kesi na kushinda pingamizi la kesi

Naomba kujua tofauti kati ya Kushinda kesi na kushinda pingamizi la kesi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwenu wajuzi wa haya mambo msaada kwenye tuta tafadhali.

Kwa mfano kesi ya Tundu Lisu Spika Ndugai ameshinda nini?

Ni hayo kwa uchache.
Maendeleo hayana vyama

cc: Pascal Mayalla, Petro E Mselewa
 
Kushinda kesi ni kushinda hukumu baada ya Jaji/Hakimu kupitia hoja, mabishano na sheria zinazo ongoza uamuzi wa Shauri zima.

Pingamizi sio hukumu bali ni uamuzi juu ya suala mahsusi lililoibuliwa ndani mwenendo wa shauri (kesi), Mfano ikiwa walalamikaji wameunganishwa kwa usahihi au ikiwa Mahakama hiyo ina nguvu kisheria kuendesha shauri husika ama hata ikiwa shauri hilo limefunguliwa kwa usahihi kisheria na kwa wakati.

Hukumu inamaliza/tamatisha shauri (kesi) lakini Pingamizi halimalizi shauri.

Kadhalika Hukumu hukatiwa rufaa au marejeo ikibidi Lakini Pingamizi Halina rufaa kama maamuzi yake hayafanyi shauri zima kutokuwa na miguu ya kusimama.
 
Back
Top Bottom