Discovery Tdi ni gari nzuri sana, nilikuwa nayo moja zamani sana Tdi II, nilikuwa natumia diesel lita 1 kwa kilomita 14.
Sijapata tena mpaka leo gari ya nguvu zake inayokula mafuta vizuri namna hiyo.
Ile ya zamani ilikuwa inanisumbuwa "rubber bushes" na "shock absorbers" mara kwa mara, mpaka nilipovumbuwa rubber bushes na shock absorbers special zinazotengenezwa kwa ajili ya 4X4 za Australia, ingawa ni ghali kidogo lakini kuzifunga nikawa nimefunga kazi. Nilikaa nazo miaka 4 mpaka nnaiuza hiyo gari sijabadilisha na bado nzuri na nilikuwa nimezunguka nayo Tanganyika nzima.