Naomba kujua ulaji wa mafuta wa Toyota Prado

Naomba kujua ulaji wa mafuta wa Toyota Prado

Bin Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
313
Reaction score
244
1582023646680.png

Habari viongozi,

Naomba mwenye ujuzi wa Toyota Prado tx 3rz, kuhusu ulaji wake wa mafuta. Mjini inatumia lita 1 kM ngapi? Na high way lita 1 km ngapi? Na kama inakula zaidi mafuta tatizo linaweza kuwa ni nini?

Ahsante.
 
Hiyo injini 3rz ikiwa haijachokonolewa na kama inatuzwa vizuri ulaji wake wa mafuta huwa ni kama ifuatavyo...

Mjini kwenye foleni ni wastani wa lita 15 kwa km 100 ambayo ninsawa na km 6.6 kwa lita moja..

High way ni lita 9 kwa km 100 ambayo ninsawa na km 11 kwa lita...

Mjini kidogo na high way kidogo (combined) ni wastani wa lita 12 kwa km 100 ambazo ni sawa na km 8.3 kwa lita moja


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi maximum speed ya kutumia hiyo km 11 kwa lita1 ni ngapi?
 
Ingia kwenye website ya Toyota Tanzania,cgagua Prado wamekuwekea kila kitu
 
Kiongozi maximum speed ya kutumia hiyo km 11 kwa lita1 ni ngapi?
Kwa wastani magari mengi yanakuwa na consumption nzuri ya mafuta kwenye high way unapokuwa angalau speed 80 mpaka 100 au 110....
Zaidi ya Speed 100, kwa magari mengi utumiaji wa mafuta huongezeka kidogo kwa sababu magari mengi speed kubwa utaendesha RPM ikiwa 3

Na unapokuwa unaendesha mwendo mkubwa let's say above 70kph, inashauriwa ufunge vioo uwashe AC ili kuserve mafuta...Upepo unaoingia kupitia madirisha jnaleta ukinzani mkubwa sana kwa injini yako.

Mwendo ukiwa chini ya 80 pia kuna uwezekano wa gari kuongeza matumizi kidogo ya mafuta...zaidi sana hizi speed 50/60 au 70 si rafiki kwa utunzaji wa mafuta coz gari nyingi hapa hasa auto zinashindwa kuvuka gea namba 3 nyingi zinachezea gia namba 2na 3..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prado TX 3rz trip ilinipa 8km/l na mishe za town kwenye foleni sana
mpaka 5km/l
 
Back
Top Bottom