Document unazotakiwa kuwa nazo ni Kitambulisho Chako chenye jina linalofanana na Document atakazokutumia, TIN number na pesa za kutolea mzigo bandarini kwa malipo ya Port charge, wharfage, shipping line, Agent fee n.k
Document atakazotakiwa kukutumia ndugu yako ni Bill of Lading, Invoice na Paking list hizo document atazipata baada ya kukamilisha kutuma mzigo kule Saud Arabia.
Utaratibu ni kwamba, wewe utamtumia jina lako kama linavyoonekana kwenye vitambulisho vyako, utamtumia address yako, namba ya sim na utamwambia utatumia bandari ipi kupokea container, huyo ndugu yako atakamilisha kutuma mzigo kwa hizo taarifa ulizomtumia kisha atapewa document ambazo atakutumia wewe kwa njia ya DHL, ukishapokea document utasubiri tarehe ya meli kufika ili uendelee na taratibu za clearance bandarini kwa container lako.
Ila ukishapokea document tafuta Clearance Agent muaminifu mapema ili aweze kuwa anakupa taarifa za tarehe ya meli ya container lako kufika.
NB:
Pia ni vyema ukaenda TRA upande wa Customs ili kujua Kodi utatakiwa kulipa kiasi gani ili kujiandaa kifedha sababu Kuna watu wameacha mizigo yao bandarini baada ya kukosa ela kulipia gharama za container bandarini.
Ila ukihitaji taarifa zaidi kuhusu hayo mambo yote nitafute ili niweze kukupa mtu muaminifu Clearing and Forwarding Agent aweze kufanya kazi yako vizuri.