Naomba kujua vigezo vya kuanzisha agrovet

Naomba kujua vigezo vya kuanzisha agrovet

Erimsi

New Member
Joined
Jan 21, 2021
Posts
2
Reaction score
0
biashara ya duka la pembejeo ili kuanza lazma uwe na vigezo gani na mtaji wa shingapi wa chini kabsa pamoja na faida zake kwa yeyote mwenye ufahamu na hili naomba kujua kutoka kwako
 
biashara ya duka la pembejeo ili kuanza lazma uwe na vigezo gani na mtaji wa shingapi wa chini kabsa pamoja na faida zake kwa yeyote mwenye ufahamu na hili naomba kujua kutoka kwako
Agrovet maana yake unataka kuchanganya Kwa pamoja madawa/vifaa vya kilimo na madawa/mifugo. Madawa ya kilimo ni bei ndogo compare na madawa ya mifugo, hivo kuvichanganya Kwa pamoja utapata faida ya kupunguza capital au ugumu wa kuongeza capital, namaanisha kama ungeuza madawa ya kilimo peke yake ungetumia pesa kidogo na kama ungeuza madawa ya mifugo peke yake maana yake ungetumia pesa nyingi

Kwa jibu jepesi ni kwamba hakuna kiwango maalumu ambacho unaweza kukadiria maana inategemea na uwezo wa mtu husika, mwingine ukimwambia mil 5 anaona ni kiasi kidogo na mwingine ataona ni kiasi kikubwa, lakini pia gharama inategemea na hiyo ofisi inakaa sehemu gani maana sehemu zingine frame ni ghari, Sana Ila Kwa mawazo yangu at least uwe na 10M

Vigezo vya kiserikali ni pamoja na duka liwe na store na lazima liwe na eneo la kupitisha hewa vizuri, kuwa na kibali cha kuuzia hayo madawa,uwe na reseni ya biashara,uwe na cheti cha daktari mwenye degree awe ndio msimamizi, uwe na muuzaji mwenye elimu ya diploma,na muuzaji awe amesajiliwa na serikali. Uwezo wangu umeishia hapo mkuu natariji umepata mwanga kidogo
 
Back
Top Bottom