Naomba kujua viwango vya presha!

Dishunga

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
276
Reaction score
58
Ndugu zangu hapa nilipo hali ya sinto fahamu, jana kwenye pita pita zangu nilikutana na mama mmoja nesi "nadhani" akiwa anawapima watu "presha ya mwili" ilikuwa maeneo ya sokoni na mimi nikavitiwa nikasogea nilipopima akaniambia nina presha 94 mimi ni mwembamba urefu 172cm uzito kama 63kgs .

Hivi hapa nilipo sijielewi hili tatizo limenipataje ilaa muda ananiwekea kipimo nilishtuka kidogo sijui kilitoa majibu sio ama vipi ila sikutaka tena kuruka tena kupima kwake.

Naombeni kujua kiwango kizuri cha presha ni kipi na ushauri nifanyaje kukaliana nalo kwa sababbu bado siumwi sehmeu yeyote.
 
kwanza umetudanganya, hakuna presha ya 94 mkuu.


normal bp ni 120/90mmhg ingawa pia ya kawaida inaweza kuanzia 100/80-139/90.


kama una bp ya 94/x ina maana ni pungufu ikimaanisha msukumo wako wa damu upo pungufu (hypotension)


hilo siyo tatizo kubwa jitahidi kunywa maji ya kutosha ili kuongeza kiwango cha maji mwilini na kupandisha presha yako.


presha yako ikishuka zaidi ya hapo utapata shoku maana uliyo nayo ilitakiwa iwe systolic reading siyo diastolic kama ilivyosoma.
 
Mkuu kupima pressure kuna vigezo vingi sana na hapo havijatimizwa.Tulia uko poa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…