Naomba kujulishwa tafsiri ya "Deni la Taifa ni Himilivu"

Naomba kujulishwa tafsiri ya "Deni la Taifa ni Himilivu"

Pamoja na kuwa CCM miaka yote hiyo bado hujui maana ya huo msamiati?

Elimu! Elimu! Elimu!
 
Japo mimi sio mchumi, deni himilivu ni deni linalolipika na nchi kuendelea kuaminiwa na kukopesheka.

Deni ambalo sio himilivu ni kufikia kiwango cha mwisho cha kukopesheka. Pale unapokopa sana huku ukuaji wa uchumi wako hauendani sambamba na uwezo wako wa kulipa madeni yako hivyo kutengeneza madeni chechefu ambayo sio tuu ni mzigo kwa taifa bali hayalipiki.

Nchi ikifikia stage hiyo, yule mkopaji anaichukua ile security yako uliitumia kukopea ama kwa kushika vitega uchumi vyako na kuviendesha yeye ili ku recovers some of the monies or kuzuia usiendelee kukopa. Ndipo hapo unasikia Mchina ameishikilia bandari fulani, au kitega uchumi fulani.

Unaweza kumsikia huyu jamaa akizungumzia deni himilivu la taifa.

P
 
CAG Assad alisema si himilivu akatishwa akaendelea kujisimamia akaitishwa zaidi bado akaendelea kuwa mzalendo wa kweli ikabidi asitafishwe ili asimuumbue malaika mkuu(shetani).
 
Japo mimi sio mchumi, deni himilivu ni deni linalolipika na nchi kuendelea kuaminiwa na kukopesheka.

Deni ambalo sio himilivu ni kufikia kiwango cha mwisho cha kukopesheka. Pale unapokopa sana huku ukuaji wa uchumi wako hauendani sambamba na uwezo wako wa kulipa madeni yako hivyo kutengeneza madeni chechefu ambayo sio tuu ni mzigo kwa taifa bali hayalipiki...
Nashukuru sana mkuu.

Nakutakia Juma Takatifu lenye baraka!
 
CAG Assad alisema si himilivu akatishwa akaendelea kujisimamia akaitishwa zaidi bado akaendelea kuwa mzalendo wa kweli ikabidi asitafishwe ili asimuumbue malaika mkuu(shetani).
No alisema deni la taifa ni himilivu ila kasi ya kuendelea kukua isipoendana na ukuaji wa uchumi, utafika wakati litakuwa sio himilivu

P
 
Mungu ni mwema wakati wote.

Kwa wale wale wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha naomba kujua tafsiri sahihi ya deni la taifa kuwa "Himilivu"

Kila zama na kitabu chake!

(Deni la Taifa ni Himilivu)​

maaana yake deni lina uwezekano wa kulipwa, izi terms mara nyingi ni kwa ajili ya kukwepa kitu kinaitwa DEPT CEILING, deni likiwa himilivu maaana yake bado una uwezo wa kukopa ingawa bado una madeni ya kulipa, Japokua katika ukweli wa uchumi duniani hauwezi kulipa deni lako lote kwa sababu unacholipa sio ulichokopa, kila mwaka kunakua na interest, ukikopa leo ulipe miaka 20 mbele maaana yake unalipa almost three times the amount you borrowed.

- kwa kifupi kabisa ni kwamba ni neno la kibepari tu ili uendelee kukopa ilihali wanajua kabisa hata ya mwanzoni huezi kulipa
 
Yaani inashangaza kuona utawala wa mkapa mpaka Jk uliacha deni la 45trilion lakini akaja mwamba Magufulu ndani ya miaka mitano tu kaacha deni 60trilioni na hakuna la maana alilolifanya likamalizika ni wizi tu na utapeli
 
Mungu ni mwema wakati wote.

Kwa wale wale wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha naomba kujua tafsiri sahihi ya deni la taifa kuwa "Himilivu"

Kila zama na kitabu chake!
Kwamba linalipika, ukicheki rasilimali na vitega uchumi tulivyonavyo unadhani vina thamani gani
 
Yaani inashangaza kuona utawala wa mkapa mpaka Jk uliacha deni la 45trilion lakini akaja mwamba Magufulu ndani ya miaka mitano tu kaacha deni 60trilioni na hakuna la maana alilolifanya likamalizika ni wizi tu na utapeli
Ngoja tupige hesabu, mradi wa Stiegler's Gorge ni trilioni 7 kama ilivyo kwa Standard Gauge. Kwa maana hiyo ni sawa kusema zimefika trilioni 60. Sasa mbona miradi haijaisha na bado tunaenda kukopa kwa Wachina na wengineo ili kumalizia?
 
Magufuli alikuwa anatuhadaa watanzania hakuwa na uzalendo wowote
 
No alisema deni la taifa ni himilivu ila kasi ya kuendelea kukua isipoendana na ukuaji wa uchumi, utafika wakati litakuwa sio himilivu

P

Ukifatilia vizuri utaona mwanzoni alisema "si himilivu", baadae alipoulizwa anyoshe ulimi akabadili gia.
 
Mungu ni mwema wakati wote.

Kwa wale wale wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha naomba kujua tafsiri sahihi ya deni la taifa kuwa "Himilivu"

Kila zama na kitabu chake!
Je tukisema "mtaji himilivu" maana yake nini?
 
Back
Top Bottom