Naomba kujuzwa asili ya neno Tanganyika

Naomba kujuzwa asili ya neno Tanganyika

lake Ngonsi

Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
13
Reaction score
48
Wanazuoni.

Naomba anayefahamu asili ya Neno Tanganyika ni ipi? Ingawa nasikia hata DRC Kuna sehemu inaitwa Tanganyika.
Wazee wa zaman au wasomi wa historia msaada tafadhari
 
Wanazuoni.

Naomba anayefahamu asili ya Neno Tanganyika ni ipi? Ingawa nasikia hata DRC Kuna sehemu inaitwa Tanganyika.
Wazee wa zaman au wasomi wa historia msaada tafadhari
Tanganyika si jina la ziwa,
Ni hivi ziwa tanganyika iliitwa tanganyika kabla ya uwepo wa nchi ya tanganyika

Ni sawa na Kenya na mlima kenya

Kulikuwa na mlima Kenya, than jina la mlima likawa la nchi

Kama tu vile kulikuwapo na mlima Kilimanjaro kabla ya uwepo wa mkoa wa kilimanjaro
 
Tanganyika inatokana na maneno mawili, Tanga na nyika. Tanga maana yake zurura, hangaika, tembea bila kufika mwisho, ukiachana na Tanga ambayo ni shuka la mashua.
Nyika ni uwanda mpana wa kisavana , walipokuja wazungu kutokana na ukubwa wa nchi hii wakaipa jina la Tanganyika, nchi ya kisavana isiyo na mwisho.
 
Kwa hiyo wazungu walikua wanajua kiswahili au sio?
 
Kwa hiyo wazungu walikua wanajua kiswahili au sio?
Wenyeji...
Wazungu hasa wajerumani walifikia Tanga...wakauliza hapa wapi ..wakaambiwa hapa Tanga....
Wakauliza tena na ukitoka hapa unaenda wapi ...wakajibiwa ahh unaenda huko Nyikani...
Ndo wajerumani wakawa Wana majina mawili ...Tanga na Nyikani...
Mwisho ndo ikawa Tanganyika..
 
Back
Top Bottom