Naomba kujuzwa bei ya bati za ALAF

B Prosper

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Posts
2,527
Reaction score
4,097
Wakuu nipo hatua ya kupaua, katika kuzunguka huko na huko kujua bati bora watu wengi wanasema ALAF, ALAF, ALAF yaani ni ALAF tu, wachache wamesema DRAGON, Dragoni baada ya kuwauliza bei yao ni 12000/ kwa mita migongo mipana 30g.

Sasa nimeshindwa kuwapata watoa huduma wa huko ALAF ili nijue bei zao. Hivyo mwenye ufahamu wa bei za Alaf anijuze tafadhali ili nifanye maamuzi
 
Kama uko dar nenda alafu kule mwenge kama unaenda kokakola mkono wa kushoto pale wanauza bei nzuri na kabla ya kununua wanakupa fundi wao anaenda kukupimia paa kabisa unanunua bati za kutosha na hazibaki
Mi nilinunua bati pale 4mtrs shilingi elfu 54000 sijajua kwa sasa kama zimeshuka bei au zimepanda
 
Asante kwa kuchangia mkuu bahati mbaya nipo ruvuma huku
 
Mkuu hiyo bei ni ya 28g au 30g
 
Mimi nilinunua bati moja kwa elfu 39 gauge 30 migongo midogo, kwa Wakala wao pale Manzese Big born, tofauti yake ikoje hapa mkuu.

Hii bei ni ya mwaka jana.
 
Alaf migongo mipana wanauza 32,000. Na me nipo kwenye atua ya kuwezeka nipo naumiza kichwa. Ila ukweli ni kuwa ALAF ni best kama unauwezo chukua hizo usijiulize mara mbili
Kabisa.Kwanza haipauki. Ila mimi nilichukua migongo midogo mipana wadau wanasema inavujisha maji ndani bora midogo, na sijaona changamoto yoyote.

Lichunguze hili kwanza ili lisije likakusumbua hapo baadaye.
 
Unahitaji mawasiliano yao nikutumie?
 
Mimi nilinunua bati moja kwa elfu 39 gauge 30 migongo midogo, kwa Wakala wao pale Manzese Big born, tofauti yake ikoje hapa mkuu.

Hii bei ni ya mwaka jana.

Tofauti migongo mikubwa na midogo wee ulinunua midogo tena wakala alikula elfu 2000 kila bati ungeenda kiwandani kojabkwa moja
 
Ila usiwaze kila sehemu hela inaliwa kama kazi yako ushamaliza sio mbaya
Yeah! Hicho ndicho kinanipa matumaini maana nilikuwa nawaza wapi nitapata kitu kizuri,kiukweli nyumba ilitoka vizuri sana, halafu hata baada ya kupungua sikurudi dar nilituma hela wakanitumia mzigo ukiwa umekamilika.
 
Tafuta wakala aliye karibu upate taarifa.

Migongo mipana kuna covermax na maxcover inatofautiana bei sababu zinatofautiana upana.

Bei itatofautiana pia kutokana na mkoa uliopo.

Huku nilipo kwa mwaka jana covermax 30g bati la 3M lilikuwa 42,000.
 
Habari mkuu,, ulishapata bati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…