Wakuu
Naomba kujuzwa bei ya engine ya Toyota Bb aina ya Engine ni 1NZA050123.
Naomba ushauri ipi nzuri kati ya injini used/mpya pia ambayo ni mswaki na ambayo ni completely
Sijaelewa hapo kwenye mpya /used.
Mpya una maana ambayo haijawahi kitumika kabisaa kama ndio basi kwa bongo hakuna labda uagize..
Au nenda toyota unaweza kupata.
Lkn kwa used zipo nyingi tuu tena zipo used za kutoka nje ya nchi dubai,japan
Na pia zipo used za ndani ya nchi used ya tandale au mabibo,mwabepande,tabata,tmk,kinondoni n.k
Uzuri wa engine inategemeana unaweza ukapata engine used ya tandake ikawa bomba zaidi ya used ya dubai..au japan.
kuhusu mswaki ni ww uamuzi wako tuu inaangalia bei unayouziwa engine complete ni bei gani na mswaki ni bei gani.
Tofauti ya bei ndio inayomata kufanya uamuzi na pili uzuri wa vitu vya kwenye engine yako mbovu ambayo unataka kuibadilisha pia vinamata.
Mfano tofauti ya labda ni laki 3.. labda engine complete ni milion 1.3 wakati mswaki ni 1M.
Mswaki unakuwa hauna coil zote 4. Alternator,starter,compresor,nozel, stering pump,wiring ya engine.
Wakati ww vitu vyako vya kwenye engine ni vibovu au hata kama vizuri ww ushakuwa na gari lazima utakuja kuvihitaji.
Mfano hapo coil peke yake ni laki 2 zote 4 kwa moja ni elfu 50 kwa bei ya chini.
Ukija otoneta si chini ya laki 1,bado starter si chini ya elfu 70 bado compressor sio chini ya laki 1 .
Hivyo uamuzi ni wako