Naomba kujuzwa bei ya Trekta za kilimo na vifaa vyake hapa Tanzania

Naomba kujuzwa bei ya Trekta za kilimo na vifaa vyake hapa Tanzania

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,184
Reaction score
5,435
Poleni na hongereni kwa majukumu yote,

Naomba kuuliza mwenye kujua bei za makampuni yanayouza trekta za kilimo majembe na hallow kwa cash na mkopo gharama zake kwa ujumla kuanzia hp 50 na zaidi.

Aina za trekta Massey Ferguson, New Holland, Ford nk.

Asanteni.
 
Kwa trekta aina ya New Holland unaweza kuwasialana na SUMA JKT pale Mwenge wanayauza au kuna kampuni inaitwa Hughes wana ofisi Arusha na pale Tazara DSM. Hao wote wanauza kwa cash.

Kama unahitaji mkopo unaweza ukawasiliana na Home.

Karibu.
 
New holland TT55 2WD ni kati ya 33.7 milioni
New holland TT55 4WD ni kati ya 41.2 milioni
New holland TT75 2WD ni 41.8 milioni
New holland TT75 4WD ni 46.6 milioni
Angalizo: hizo ni bei za trekta tu bila mitambo ya ziada kama jembe au harrow na unalipa cash
 
Massey mpya utapata za Pakistani na zenyewe bei zake zinapita humo humo kwenye new holland, bei inabadilika kutokana na nguvu (Hp) na kama 2wd au 4wd. Massey mpya ya uingereza zipo very advanced and very expensive too.

Ford mpya nazo ni very advanced and expensive too.

Angalizo: kama pesa inaruhusu ni vema kununua trekta jipya siku zote
 
Massey Ferguson zipo tofauti tofauti 2WD & 4WD nyingi zinaenda hadi É17,000 mfuko wako unaongea tu mkuu
 
Back
Top Bottom