Mataka taka aya
My Take ya Taa
Taa zote za booster zinazouzwa mtaani sijui zima feni sijui angel Eye blah blah it is nothing compared na taa original zilizokuja na Gari....
Gari zimetengenezwa kwa features kulingana na mazingira husika. Huo mwanga wa rangi ya unjano sio sahihi kwa mazingira yetu. Hata zile fog light pia si sahihi kwa mazingira yetu ya afrika especially tanzania.
Hizo taa zinaitwa taa za aina ya Halogen..... Mwanga wake huwapa shida sana watu wengi kuona usiku.
Unavyosema mwanga wa taa za kisasa hizi zinatoa LED au White blue sio sahihi na ni makosa sio kweli.
Mimi nimefunga hizo taa kwenye gari ya awali na hii ya sasa ni nzuri sana na zina angaza vizuri sana especially mashimo kwenye baadhi ya barabara.
Kuhusu kuuumiza macho watumiaji wengine ni matokeo ya namna umeset ile beam ya headlights. Unatakiwa upaki gari kisha set muale wa taa usiwe straight ulenge sakafu au barabara unapokuwa umewasha katika lower beam, na iset ipige straight katika high beam.
Madereva wengi wa tanzania miaka hii nimegundua hawapo makini na taa zao wanapotembea nyakati kiza kikiingia. Mtu anatembea taa amewasha full..... Hii si sawa kabisa. Si sahihi.
Kwann uwashe taa full beam na ukijua wazi unawalenga wenzako usoni. Kuna baadhi ya magari kama descovery 4 huwa yana sensor za mwanga kwenye headlights kusaidia madereva wanaojisahau kushusha beam pale wanapokuwa wanamulika wenzao mbele yao.
Inajideam yenyewe automatically ukishapishana inapandisha kurudisha high beam. Ni swala la vipimo tu ila sio kosa la hizo bulb.
Kama umefuatilia hata taa za barabara za usiku hizi za kisasa zinakuja na huu mwanga wa white blue sababu unaangaza vema zaidi na kupunguza sana majanga. Yale mataa ya zamani ya barabara ya Halogen hata yakiwashwa huwezi kuona msaada wake maana yanakuwa yanawaka bila kuangaza.
Kuhusu faida hizi bulb za LED zina faida mara dufu.
1. Zina tumia moto kidogo sana kwa maana haziwi mzigo katika battery ya gari.
2. Hazina joto hivyo husaidia kioo cha taa kubwa za mbele kutokufubaa. Taa zile za mwanga wa njano zina joto sana na umeme zinatumia wa ziada. Lile joto huwa linafanya ile surface ya kioo cha taa kubwa kulainika na wakati gari ikitembea vumbi na uchafu huwazinashikamana na hiyo surface na kufanya ipoteze mng'ao wake na kufubaa. Labda kama hiyo gari inatumia headlights zenye materials ya glass na sio plastic.
3. Baadhi ya hizi bulb huwa na feni so husaidia zidumu na kuwa imara muda mrefu bila kuungua. Sababu haziwezi kupata reaction kutokana na over heating.