1.Nipo arusha
2.Nina familia
3.Matumizi yangu ni kwenda kazini na kurudi
4.Tutatumia kama usafiri wa familia
5.Ni mara yangu ya kwanza kumiliki gari
Sent from my SM-A145F using
JamiiForums mobile app
Mimi ninayo Alphard mwaka wa 5 huu.. Ni nzuri sana.. Chukua cc 2360 usinunue yale yana kama pampa limeshuka mpaka chini noo.. Yale yanachakaa haraka bodi lake.
Hata bei yake daima ni chini kuliko Alphard Nyingine.
Suala mafuta ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko kiuchumi..
Inafaa sana ukitumia peke yako, familia au hata kikundi maana ina siti 8.
Viti vyake unavigeuza upande unaotaka.. Unaweza ukaweka kiofisi, ki conference, ki luxury, kubwa kuliko vile viti ni vitanda vizuri sana yaani ukikunjua unalala kama nyumbani tuu.
Ukiwa na safari au misibani au piknik huhitaji kutafuta lodge unaweza kulala kwa raha kabisa hata watu 3.
Ukikunja viti vya nyumba unabeba mzigo kama wa kirikuu na ukikunja na vya katikati ni balaa kirikuu haioni ndani, full tinted unapita unampungia mkono trafic.
Kwa uzoefu wangu ile gari ina matumizi mengi sana sana ni vile utakavyoamua au kutokana na mazingira ya wakati huo.
Huwezi juta hata siku moja kuwa Alphard.. Kwanza ni kubwa na pana sana mule ndani.. Dereva unakaa kwa nafasi na paa la juu bado lipo mbali huwezi gusa kwa kichwa.
Kwa nje linaonekana kama lipo chini lakini ndani lipo juu sana.
Kama ukinunua yale ambayo ground clearance yake ni ndogo.... Simpo tuu ni kwa mafundi wanakuwekea Spencer za inch moja moja au moja na nusu inakuwa juu vizuri.
Mimi napita nalo popote vumbi, au barabara nzuri, makorongo, mashimo popote, milima, au mabonde.
Service fuata oil sahihi ya engine 10w30 na gear box type iv.. Mengine kawaida.