Naomba kujuzwa dawa bora kwa ajili ya kutibu mafua ya Kuku

Naomba kujuzwa dawa bora kwa ajili ya kutibu mafua ya Kuku

phael vet

Senior Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
132
Reaction score
89
Habari waungwana naomba kuuliza kwa anaejua dawa bora ya kutibu Mafua ya kuku.
 
Dawa nzuri ni Tyrodox Extra, ila fanya usafi wa banda hakikisha hewa inapita na kutoka, hakikisha hakuna vumbi bandani.

Dawa sio kinga bila kuzingatia usafi utawaua kwa madawa.
 
Tylodox ni nzuri sana, lakini siku hizi naona zinasumbua kupatikana.
 
Fluban uhakika. Ila kama alivyosema mchangiaji hapo juu usafi wa banda muhimu. Hakikisha unabadilisha maranda kila baada ya miezi 2 au 3. Mzunguko wa hewa pia muhimu sio kuku wanafichwa kama utumbo
Kweli kinga ni bora sana kuliko tiba.
 
Dah mafua yakianza, dawa ni kupumzisha banda maana hupona na kurudi ndani ya wk 1 tu.
 
Wanyweshe maji yaliyochanganywa na pilipili kichaa iliyopondwa, tumia bomba la sindano!

Zingatia usafi wa banda, na hakikisha kuna hewa ya kutosha.

Everyday is Saturday..............................😎
 
Ushawahi kutumia dawa za kienyeji zinazotokana na majani na viungo vya chakula?
My friend mafua yakishakuwa critical hizo dawa za kienyeji huwa hazifunction kabisa, na hata za dukani tylodox ndio huwa inatibu.. Hizi fluban hamna kitu
 
My friend mafua yakishakuwa critical hizo dawa za kienyeji huwa hazifunction kabisa, na hata za dukani tylodox ndio huwa inatibu.. Hizi fluban hamna kitu
Mimi hufuga broilers, ninachokifanya naanza kuwapa since day 2 mpaka mwisho kwa hiyo mafua hayapati nafasi.
Tupunguze chemical kwa kutumia mitishamba
 
Mkuu nikupe mawasiliano ya dr wa mifungo ambaye anadeal na products za kuku na anawajua kuku vizur.!! ukiwa tayar sema nikupe
 
... hii kitu inayoitwa mafua ya kuku ilinifanya nikaachana na ufugaji wa hao viumbe. Ni kero sana.
 
Back
Top Bottom