Naomba kujuzwa dawa ya jino bila kun'goa

Huenda shida haiko kwenye jino.

Umesoma nilichoandika awali
Ndio hivyo nakwambia. Mie nliwahi kuumwa nikawa nafikiri ni jino kumbe fizi zilikua na shida. Sasa kama wewe meno yako yanang'oka tu huoni utakua na shida nyingine. Kinywa kina mambo mengi sio kila maumivu ni jino
 
Basi na mimi nitafariki maana meno yangu karibu yote ni mabovu huwa yanalegea bila kuuma na kutoka yenyewe ila hili linauma na Kuna lingine ukiligusa linauma pia
Kama upo Dar,nenda buguruni kwenye mataa yanayounganisha barabara inayotokea Ilala na ile ya Mandela,ukiwa kwenye hiyo junction unapokuwa unatokea Ilala mkono wa kushoto kuna watu wanauza madawa ya asili,kajipatie dawa ya meno pale hutahitaji kung'oa.
 
Kuna dawa Moja ipo kama CHUMVI ya mawe!
Bahati mbaya nilipewa Zambia, na hawakunambia inaitwaje lakini nasikia hata Tanzania ipo.
Unaweka Hilo jiwe linalofanana na CHUMVI, Kisha mdomo wote una chachuka na kushika ganzi
Ukifanya hivyo mara 3 umepona kabisa, nitaulizia jina
 
Duh
Watu waliopona dawa hawazikimbuki jmn
 
Kuziba inategemea na stage ikishakuwa severe huwez ziba na inategemea limetoboka upande gan ,pia kuziba pia kuna Aina kuna ya mda mref na mfup ya mda mref garama ni kubwa
 
Nikushauri nenda kasafishe halafu uzibe acha na hizi dawa temporary , kikawaida jino likishakuwa na tundu basi kuendelea kuchimbika ni rahisi mno maana kusafisha chakula kinachoingia ndani ya tundu inakuwa ngumu hivyo ni bora uende hospitali ukasafishwe kitaalamu halafu wakuzibe .

Baada ya hapo nikushauri pia ununue dawa ya meno ya sensodyne au colgate max fresh na uwe unasafisha meno yako angalau mara mbili kwa siku yaani asubuhi na kabla ya kulala na usile chochote wala usinywe kinywaji chochote (ispokuwa maji) unapotaka kulala .

Kingine jiepushe na matumizi ya vitu vyenye sukari nyingi iwe mchana au usiku na kama ikatokea umetumia kitu chenye sukari nyingi basi sukutua kwa maji safi ili kuondoa sukari mdomoni.

Namna ya kusafisha meno
1. Ukishaweka dawa kwenye mswaki usiuchovye kwenye maji piga hivyo hivyo .

2. Safisha upande wa nje wa meno kwa utaratibu ukijitahidi kupitisha mswaki karibia na fizi pia utafanya hivyo hadi kwenye meno ya mwisho (magego).

3. Safisha upande wa ndani wa meno hakikisha pia unasafisha hadi karibu na fizi na unaenda hadi kwenye meno ya mwisho (magego).

4. Safisha upande wa meno unaotumia kutafunia hakikisha unaenda hadi meno ya mwisho ( magego).

5. Safisha ulimi

6. Fanya hivyo kwa meno ya chini na ya juu .

7. Hakikisha unakaa angalau dakika moja au zaidi kabla ya kusukutua mdomo kwa maji safi.

N.b
Inavyoonekana jino lako limelika hadi kufikia stage ya kuguswa nerve ndiyo maana linauma wakati tu wa kula au kunywa na si muda wote hili linazibika bila root canal (ila fuata jinsi daktari wako atakavyokushauri).

Wahi mkuu kabla haujalipoteza.
 
Duh
Watu waliopona dawa hawazikimbuki jmn
[emoji23][emoji23][emoji23] kweli hatuzikumbuki hii anayo semea wakati mdogo niliwahi wekewa, jino lilikua limetoboka, ilikua mbeya hiyo mwaka 2000, ila sikujuaga hata ina itwaje lilikua jiwe tu kama la chumvi, kikubwa baada ya kuwekewa sikuumwaga tena jino

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…