Naomba kujuzwa gharama za kufunga mtambo wa Bayogesi na nishati nyingine mbadala

Naomba kujuzwa gharama za kufunga mtambo wa Bayogesi na nishati nyingine mbadala

Chrysanthemum

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
1,531
Reaction score
5,787
Habari wanajukwaa:

Kama mnavyotambua na kuelewa ni nchi yetu na Dunia kwa ujumla tuko katika kampeni ya matumizi ya nishati mbadala kama bayogesi, umeme na Gesi nyinginezo ili kukwepa matumizi ya kuni na mikaa kupunguza uharibifu wa mazingira.

Wataalamu na wazoefu wengine ambao pengine mmefunga nyumbani au kwenye taasisi tusaidieni kupata gharama za kufanya hii kitu.

1. Kufunga mtambo wa Bayogesi kwa raia labda kwa matumizi ya nyumbani tu nini kinahitajika na gharama zake zikoje ?

2. Kufunga mtambo kwa Taasisi zenye watu wengi mfano shule labda kwa matumizi ya kupikia chakula cha wanafunzi Kuanzia 600-1000 gharama zake zikoje na nini kinahitajika?

Pia wakati natafuta majibu kuna mtu alinipa idea ya kutumia hii gesi ya kawaida tunayotumia majumbani kama ORXY , Mihan n.k kwamba kuna wataalamu pia wanaofunga hizi gesi kwenye taasisi zenye watu wengi kama shule na hospitali ila unaongea na kampuni mfano ORXY wanakuuzia mtungi mkubwa zaidi labda lita 200 n.k wao wanafanya installation za vifaa mpaka jikoni ikishakamilika wao watakua wanakuuzia Gesi tu, Tafadhali kama kuna mtaalam atusaidie hapa!

Hivyo hivyo wadau tukiachana na hiyo Bayogesi, je kwenye matumizi ya umeme wa TANESCO tunawezaje kuutumia huu ememe kwenye kupika chakula cha watu wengi mfano shuleni , hospital au kwenye shughuli ?
Je kuna majiko makubwa ya umeme ya kuweza kuandaa chakula cha watu 500-1000 au vifaa au vyombo vikubwa kama hizo Rice cooker 🤣 zenye kuweza kupika hadi kilo 80-100 za mchele au maharage ?

Hii mada itawafaidisha wamiliki wa shule , Hospitali , Kambi za Jeshi, Magereza n.k

Karibuni sana wataalam.
 
Biogas hii technology wengi hawaijui TZ, hawaitumii, lakini ni Nzuri sana katika matumizi ya majumbani. Haichafui mazingira (eco-friendly) na renewable source of energy.
VITU Muhimu:
  • Digestor
  • cow dung
  • Gas stove
  • Pipes
  • etc, vingine wataongezea wengine.
Kumbuka: Digestor inaweza Kutengenezwa locally (using simtank or pit hole) au ya kununua.
==========
Hayo ndiyo niyajuayo kuhusu Mimi.
 
Biogas hii technology wengi hawaijui TZ, hawaitumii, lakini ni Nzuri sana katika matumizi ya majumbani. Haichafui mazingira (eco-friendly) na renewable source of energy.
VITU Muhimu:
  • Digestor
  • cow dung
  • Gas stove
  • Pipes
  • etc, vingine wataongezea wengine.
Kumbuka: Digestor inaweza Kutengeneza locally (using simtank or pit hole) au ya kununua.
==========
Hayo ndiyo niyajuayo kuhusu Mimi.
Asante sana mkuu Blue Bahari angalau tumejua mahitaji , vipi kuhusu gharama mchanganuo kidogo hata kwa kugusia ufungaji ?
 
Biogas hii technology wengi hawaijui TZ, hawaitumii, lakini ni Nzuri sana katika matumizi ya majumbani. Haichafui mazingira (eco-friendly) na renewable source of energy.
VITU Muhimu:
  • Digestor
  • cow dung
  • Gas stove
  • Pipes
  • etc, vingine wataongezea wengine.
Kumbuka: Digestor inaweza Kutengenezwa locally (using simtank or pit hole) au ya kununua.
==========
Hayo ndiyo niyajuayo kuhusu Mimi.
Niliendaga lutindi mission tanga nliona wao wanaitumia

Ova
 
Niliendaga lutindi mission tanga nliona wao wanaitumia

Ova
Asante sana mkuu, ni kitu nzuri sana shida tunakosa mtu wa kutudadavulia kidogo ufungaji na gharama zake ! Kama ilivyo michango kwenye ujenzi wa nyumba watu walivyo na madini!

Hata kama kuna kampuni zinazohusika waweke maelezo na mawasiliano ikiwezekana!
 
Asante sana mkuu, ni kitu nzuri sana shida tunakosa mtu wa kutudadavulia kidogo ufungaji na gharama zake ! Kama ilivyo michango kwenye ujenzi wa nyumba watu walivyo na madini !!
Hata kama kuna kampuni zinazohusika waweke maelezo na mawasiliano ikiwezekana !!
Tuwasubirie wataalam waje

Ova
 
Nyumbani kwetu tulifunga mtambo wa cubic meter 13, kwa gharama ya milioni tatu

inauwezo wa kuwasha majiko plates 4 za gas kwa masaa 12 kwa siku bila kuzima
 
Biogas ni methane gesi ambayo inaweza kuwaka / kutumika kama nishati, vitu vikioza, vinyesi n.k. vinatoa hio biogas, kwahio unachohitaji ni digester (iwe pipa shimo au chochote kile) so long as utaweka favorable condition ya mabaki kuoza basi utapata biogas, (methane)

Wengi wanatumia kinyesi cha Ng'ombe lakini hata cha binadamu kinaweza kutoa biogas ila kupata kinyesi cha watu cha kutosha to make it worthwhile..., labda kwenye magereza au mashule.....

Lakini kwa Tanzania hio ni waste of time (unless unamabaki mengi kwahio unataka kuyabadilisha kuwa mbolea) hivyo moto / nishati iwe secondary... Ila ukitaka unaweza kwa kutumia pipa ukatengeneza biogas plant wala huitaji gharama kubwa zaidi ya pipa na tubes za hapa na pale

Tanzania tuna mbadala wa kutosha ambao una ufanisi zaidi na unaweza ukafanya kila mtu akapikia kwa gharama nafuu zaidi

 
Ninapofanyia kazi wanapika kwatumia umeme na wanalisha zaidi ya watu 2000 per day. Kama utapata watu wa Ako company hii inajihusisha na chakula hasa migodi mikubwa
Mkuu tusaidie hata kuangalia hizo sufuria zao za umeme zikoje zikoje ! Utuelezee kidogo na namna ya kuzipata !!
 
Back
Top Bottom