Naomba kujuzwa gharama za kutengeneza sakafu rafu

MalaikaMweupe

Member
Joined
Feb 24, 2009
Posts
72
Reaction score
18
Habari za humu wadau?

Msaada wenu tafadhali.

Ninahitaji kupiga rafu sakafu, fundi kanambia labour charge ni sh 800,000/ ambapo ataongeza kifusi chini kidogo kunyanyua, maana kilikuwa kimeshawekwa kitambo na kazi inayobaki ya rafu, gharama yake ndo kanambia laki8, mimi nmeona ni parefu sana.

Mnasemaje?

Ushauri wenu pliz
 
Mbona umeandika nusu nusu Kiongozi?

Hiyo rough unayosema ni kwa Ukubwa upi wa nyumba yaani nyumba ya vyumba vingapi?

Na hiyo rough yenyewe inajazwa kwa unene upi (thickness)

Ukiona ina kukata si uombe akupunguzie
 
Habari za humu wadau?
Msaada wenu tafadhali. Ninahitaji kupiga rafu sakafu, fundi kanambia labour charge ni sh 800,000/ ambapo ataongeza kifusi chini kidogo kunyanyua, maana kilikuwa kimeshawekwa kitambo na kazi inayobaki ya rafu, gharama yake ndo kanambia laki8, mimi nmeona ni parefu saaaaanaaaaa.........mnasemaje? ushauri wenu pliz
Kama unaona hela ni nyingi, fanya wewe mwenyewe
 
Mbona umeandika nusu nusu Kiongozi?

Hiyo rough unayosema ni kwa Ukubwa upi wa nyumba yaani nyumba ya vyumba vingapi?

Na hiyo rough yenyewe inajazwa kwa unene upi (thickness)

Ukiona ina kukata si uombe akupunguzie
Nyunba ya vyumba 3 vya kulala vya wastani tu, sebule dining room, study room, bafu2 jiko na korido
 
Habari za humu wadau?

Msaada wenu tafadhali.

Ninahitaji kupiga rafu sakafu, fundi kanambia labour charge ni sh 800,000/ ambapo ataongeza kifusi chini kidogo kunyanyua, maana kilikuwa kimeshawekwa kitambo na kazi inayobaki ya rafu, gharama yake ndo kanambia laki8, mimi nmeona ni parefu sana.

Mnasemaje?

Ushauri wenu pliz
Elfu 20 kwa chumba 3mx3m
 
Hao vibarua kwa kazi ya Zege hulipwa 25,000 hadi 35,000 kwa siku.

Chukulia wapo 10

Msimamizi wao, yaani fundi Kiongozi analipwa 50,000 hivyo kwa kazi yote jumla muombe aifanye kwa 400,000 isizidi 500,000

Nyunba ya vyumba 3 vya kulala vya wastani tu, sebule dining room, study room, bafu2 jiko na korido
Mpe 200,000 maximum 300,000. Hataki tafuta mafundi wengine. Laki 8 ni pesa ya kujenga boma la hiyo nyumba yako.
 
Hao vibarua kwa kazi ya Zege hulipwa 25,000 hadi 35,000 kwa siku.

Chukulia wapo 10

Msimamizi wao, yaani fundi Kiongozi analipwa 50,000 hivyo kwa kazi yote jumla muombe aifanye kwa 400,000 isizidi 500,000
Wapi huko fundi analipwa 50k kwa siku? Au saidia zege 35k?
Ukilipa fundi zaidi ya 20k na saidia zaidi ya 10k umepigwa.
 
Huenda nilipigwa

Ila kazi ya zege nimewahi kulipa 25,000 kwa kichwa na walikuwa vijana 25 maana ilikuwa zege ya slab ya ghorofa ( 4th floor) na ilikuwa wanabeba kwa kichwa.

Gharama inategemeana na bargain power yako
 
Fundi wa kawaida aliyeitwa na fundi mwenzie ni 25k, msaidizi ni 15k. Malipo yakiwa 20k kwa 10k kuna baadhi ya gharama zao utazibeba (misosi n.k.)
 
Wapi huko fundi analipwa 50k kwa siku? Au saidia zege 35k?
Ukilipa fundi zaidi ya 20k na saidia zaidi ya 10k umepigwa.
Upo mkoa gani, ambako ukimlipa fundi zaidi ya 20k perday utakua umepigwa ?
 
Huenda nilipigwa

Ila kazi ya zege nimewahi kulipa 25,000 kwa kichwa na walikuwa vijana 25 maana ilikuwa zege ya slab ya ghorofa ( 4th floor) na ilikuwa wanabeba kwa kichwa.

Gharama inategemeana na bargain power yako
Huenda hukupigwa pia. Wewe ndio uliona ugumu wa kazi,though ulichangia kwa kutoa fedha. Kiujumla hakuna guarantee ya malipo kwa fundi kama sheria.
Ukiona inamfaa,mpe hata zaidi ya hiyo uliyotoa!
 
Umenena vyema, niliona ugumu wa kazi yao ndiyo maana niliridhia kuwalipa kiasi kile.

Imagine mnaanza kazi ya zege saa 1 asubuhi na ilikuja kukamilika saa 12:30 jioni
 
Back
Top Bottom