Naomba kujuzwa gharama za kuweka Gypsum katika nyumba

Naomba kujuzwa gharama za kuweka Gypsum katika nyumba

Mkohoti

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
1,857
Reaction score
2,919
Habarini wadau,

Kama mada ilivyojieleza. Naomba kujua kwa nyumba yenye sebule, dining, jiko, vyumba viwili na master. Kwa makadirio inaweza ikacost shilingi ngapi kuiweka Gypsum. Na ni Gypsam board gani nzuri na cost ni shilling ngapi?

Natanguliza shukran.
 
Inategemea na sqm za nyumba yako. Board moja inauzwa 14,000-22,000/- muulize fundi nyumba yako inahitaji board ngapi.
Thanx mkuu, ngoja nitamcheki. May be kwa uzoefu wako kwa nyumba kama hiyo makadirio tu.
 
Thanx mkuu, ngoja nitamcheki. May be kwa uzoefu wako kwa nyumba kama hiyo makadirio tu.
Ngoja nikapitie rekodi zangu. Kuna uzi humu niliweka jinsi gani ufanye utumie boards chache ngoja niutafute
 
Jinsi ya kupunguza gharama za gypsum board.
Piga hesabu unahitaji boards ngapi. Mfano unahitaji 50pcs. Nunua 20pcs kwanza. Mwambie fundi aweke nzima nzima,yaani aweke sehemu zinazoingia nzima nzima nyumba nzima. Zile sehemu zinazohitaji vipande aziache kwanza.
Utashangaa nzima zinaingia 20 au pungufu.
Zile sehemu zinazohitaji vipande nenda hardware ongea nao wakuuzie damaged boards(hizi huwa zinakuwa zimemeguka kidogo wakati wa kumshusha mzigo hawawezi kuuza kwa wateja wa kawaida) hizo utauziwa moja 5000-7000. Unanunua kama 30pcs ndio unaenda kuweka sehemu zinazohitaji vipande.
Hesabu iko hivi
Boards nzima 50 ni 50*14,000=700,000
Kwa njia hii nilioshauri
Board nzima 20 ni 20*14,000=280,000
Damaged board 30*6000=180,000
Total 460,000
700,000-460,000=240,000
Umeokoa 240,000.
Hope ni hii, asante
 
Habarini wadau, kama mada ilivyojieleza. Naomba kujua kw nyumba yenye sebule, dining,jiko ,vyumba viwili na master. Kwa makadirio inaweza ikacost shilingi ngapi kuiweka Gypsam. Na ni Gypsam board gani nzuri na cost ni shilling ngap?

Natanguliza shukran.
Kaka tuwasilia ili ofisi ya UVIMO ikiwa ni umoja wa mafundi ujezi wakupe makadirio hayo, ikibidi utupe kazi tukufanyie kwa bei ya kawaida na kwa ubora .

UVIMO mawasiliano
0753961896
0629361896
0753927572- wasap
 
Unahitaji board 25 (7×4 ft each)na mikanda kama 40 (7 ft each) bei inategemea ulipo
 
Kaka tuwasilia ili ofisi ya UVIMO ikiwa ni umoja wa mafundi ujezi wakupe makadirio hayo, ikibidi utupe kazi tukufanyie kwa bei ya kawaida na kwa ubora .

UVIMO mawasiliano
0753961896
0629361896
0753927572- wasap
Ok. kaka siku nikianza nitakucheki kuangalia bei zako zimesimamaje. Hope upo Dar.
 
Ninepiga gypsum 2 rooms za nyumba ya nyuma: kuanzia blundering, kupiga gypsum, mikanda, na kuvipiga skimming na rangi (rangi ya maji nyeupe then cream) aisee milioni moja imeisha.
 
Habarini wadau,

Kama mada ilivyojieleza. Naomba kujua kw nyumba yenye sebule, dining,jiko ,vyumba viwili na master. Kwa makadirio inaweza ikacost shilingi ngapi kuiweka Gypsam. Na ni Gypsam board gani nzuri na cost ni shilling ngapi?

Natanguliza shukran.
Samahani Mkuu. Ulifanikiwa kutumia gypsum board ngapi katika Site yako? Na gharama kwa moja inauzwaje? Naomba kufahamu maana na mimi natarajia kuzifunga sio muda mrefu na specification za nyumba yangu naona zinaendana kiasi na yako
 
Tusaidiane pia makadirio ya bei za kufunga board. Inafungwa kwa room au kwa board? Gharama zikoje roughly?
 
Back
Top Bottom