Naomba kujuzwa historia ya Palestina na Israel

Naomba kujuzwa historia ya Palestina na Israel

Joined
Aug 7, 2020
Posts
9
Reaction score
9
Jaman naomba Msaada kwa anaejua vizuri chimbuko la haya mataifa vizazi na vizazi pia yupi mwenyehaki pale.
 
Eti parestina!!!!!????
Pumbafffff
 
Jaman naomba Msaada kwa anaejua vizuri chimbuko la haya mataifa vizazi na vizazi pia yupi mwenyehaki pale.
Nitajaribu kufupisha:
Mwaka 70 AD, wayahudi wakiwa chini ya utawala wa kirumi walichoka kutawaliwa.
Wakaanzisha vurugu dhidi ya dola ya kirumi ili wapewe uhuru wao, vurugu hizo zilipelekea Warumi kukasirika na kuishambulia Israel vibaya na kuangamiza kabisa mji wa Yerusalemu.

Maelfu ya wayahudi walipoteza maisha na mamilioni walikimbia makazi Yao na kwenda kuzaliana mataifa mengine duniani kama wakimbizi.

Kufikia karne ya tano 500 AD baada ya dola ya kirumi kuanguka, Jimbo(taifa) la Yuda au Israel ambalo awali lilishikiliwa na Warumi, liliangukia mikononi mwa Caliphates au Sultanate za kiarabu na baadae Ottoman empire(Uturuki) mpaka miaka ya 1920 ndipo waingereza wakalichukua. Muda wote huo Israel ikiwa chini ya waarabu iliitwa Palestina na waarabu waliohamia na kuzaliana hapo waliishi Kwa amani na wayahudi waliobakia tangu kuanguka Kwa Jerusalem 70AD.

Utata ulianza mwaka 1948 baada ya Uingereza kuamua kuwarudisha wayahudi wote waliokuwa Ujerumani wakinyanyasika na kuuwawa na Hitler. Walipofika Palestina, walipewa maeneo ya kusettle na kufanya shughuli zao lakini wapalestina hawakupenda hivyo wakapanga mikakati ya kuwashambulia wakishirikiana na mataifa jirani ya kiarabu (the first Israel Arab war) Israel ilishinda kwenye vita hiyo na hatimae kuwapola maeneo zaidi na kutanua mipaka Yao.

Palestina hawakukubali wakajipanga tena miaka ya sitini lakini Kwa mara nyingine wakapigwa na kuporwa maeneo zaidi hatimae ikabaki Gaza na West Bank kama unavyoona leo.
 
Back
Top Bottom