NB: Wingi au uchache wa maswali haukupi ushindi mahakamani.
MUHIMU: Uliza maswali yatakayokujengea umiliki wa ardhi husika yaani maswali yatakayokuwa na faida kwako hasa juu ya kiini cha mgogoro na umiliki.
Mf. Ulivyopata umiliki, Ukubwa wa eneo, umeoa au kuolewa na mwaka gani, eneo lilipo na vitu kama ivyo.
Usilipe Baraza kazi kuanza kufikiria na wewe umelenga nini, jambo muhimu ni uliza maswali wazi kabisa usilete kona kona hazina maana kabisa.
Ungefafanua kidogo ishu yako ungepata mengi zaidi, ila hayo zingatia.
MWISHO: Fahamu kuwa Baraza la Kata halina mjumbe yoyote ambaye ni mtaalamu wa sheria kwaio kuwa wazi na jitahidi ueleweke sana sana sana.