Naomba kujuzwa jambo kuhusu dhamana, hasa ya fedha taslimu

Justine_Dannie

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
1,962
Reaction score
1,618
Habari wakuu na madogo.!
Naomba kujuzwa jambo kuhusu dhamana, hasa ya fedha taslimu.
Ipo taratibu ya mahakama kuhusu kuwaachia watuhumiwa wa makosa fulani fulani kwa dhamana ya pesa.
Hali hii inawafanya watuhumiwa kua huru wakati wakiendelea kusubiria mashauri yao wakiwa uraiani (nje).
Swali langu ni je nini kinafuatwa pale mtuhumiwa anaposhinda kesi!?
Je pesa zilizotumika kama dhamana zinarudishwa endapo itaamriwa mtuhumiwa hana kosa!?
Asanteni.
 
mmmh kurudishwa sidhani
Mali ikienda kwa mganga hairudi
 
Dhamana huwa inarudishwa baada ya hukumu kutolewa.

Ikitokea mtuhumiwa amekimbia au kutofika mahakamani dhamana hiyo huweza kubatilishwa na mtuhumiwa kufunguliwa kesi nyingine ya kutokuhudhuria mahakamani.
 
..."inarudishwa baada ya hukumu kutolewa,
Je zinarudishwa bila kujali ni guilty or not guilty!?
 
..."inarudishwa baada ya hukumu kutolewa,
Je zinarudishwa bila kujali ni guilty or not guilty!?
Yeah haijalishi. Dhamani huwa ni 'bond' inayowekwa kati ya mahakama na mtuhumiwa. Hii husaidia kumfanya mtuhumiwa asiikimbie mahakana na pia kumweka mtuhumiwa huru wakati kesi ikiendelea.

Kama kesi ikiisha na hukumu ikapitishwa akawa guilty ina maana ata serve sentence atakayopewa au kama sio guilty basi ataachiwa huru.

Ina any case bond lazima irudishwe kwakuwa haihusiani na mtuhumiwa kukutwa guilty or not guilty. Bond ilokuwa inamfanya tu asiikimbie mahakama na pia awe huru kufanya mambo yake mpaka hapo hukumu itakapopitishwa.
 
Nimekuelewa vizuri Sana,
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…