Naomba kujuzwa jinsi ya kutengeneza mishumaa

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Kama kichwa cha habari kisemavyo ningelipenda kufahamu utengenezaji wa mishumaa materials manunuzi utengenezaji mpaka faida toka kwa mwenye uelewa asanteni
 
kama kichwa cha habari kisemavyo ningelipenda kufahamu utengenezaji wa mishumaa materials manunuzi utengenezaji mpaka faida toka kwa mwenye uelewa asanteni

Uko wapi? Umejiandaa kulipia mafunzo haya ama malipo kwa Mungu? Funguka
 
slim5 kulipia kusoma sio issue. issue ni je ni kazi inayolipa ukizingatia making means manufacturing / je itanilipa ? ni tofauti na biashara ya uchuuzi
 
Last edited by a moderator:
slim5 kulipia kusoma sio issue. issue ni je ni kazi inayolipa ukizingatia making means manufacturing / je itanilipa ? ni tofauti na biashara ya uchuuzi

Kwa skills hizi, nilitegemea ujiajiri
 
Last edited by a moderator:
slim5 kulipia kusoma sio issue. issue ni je ni kazi inayolipa ukizingatia making means manufacturing / je itanilipa ? ni tofauti na biashara ya uchuuzi

Ni rahisi sana kutengeneza mshumaa!

Japo mimi nimegharamika cost kibao tu za kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali wa vitu mbali mbali lakini naweza kukusaidia highlights....

Mshumaa unatengenezwa katika maumbo mbali mbali kama wewe tu unavyopenda, pia na rangi...

Mishumaa inaweza kuwa ya:

1.kuweka chooni kupunguza harufu na kuleta mandhari nzuri (Hapa kuna kemikali inayochanganywa kwa ajili ya kupunguza harufu, kuna perfume yake maalum)

2. Kuweka chumbani kwako kwa ajili ya matumizi yako na mwandani wako kama unae. Hapa napo kuna mchanganyiko wake unaotakiwa.

3. Mishumaa mingine ipo kwa ajili ya mapambo katika maeneo maalum kama KANISANI, SEBULENI na mishumaa vile vile inaweza tumika msibani.. matumizi yanatofautiana tu kulingana na mahitaji....

Kama nilivyozungumzia suala la rangi ya mshumaa, umbo na eneo unalotakia kutumia, hivi vitu ni muhimu sana kutambua ili ujue mshumaa wako uutengeneze katika umbo la aina gani.

Kuna mishumaa ambayo ni kwa ajili ya luxury tu ndo maana tunaona inakuja na maumbo ya kupendeza na kuvutia sana! Hiyo ni gharama kubwa kui design na kuifikisha sokoni kwa mlaji...

Mishumaa ambayo inaenda kwa mlaji (consumer) ambayo ni ile midogo midogo myeupe, ni rahisi sana kuitengeneza kwa sababu haihitaji mambo mengi....

NB: Mshumaa unaweza kuutengeneza hata kwa dakika 10 tu ukiwa mtaalam hasa! Ni jambo tu la kucheza na kemikali na kama una malighafi zote zinazohitajika.

Nitarudi baadae kwa ajili ya kukufundisha zaidi juu ya mahitaji muhimu ya kutengenezea mishumaa, jinsi ya kutengeneza katika maumbo mbali mbali na mpaka namna ya kuifanyia upakiaji mpaka kuifikisha sokoni...

Asante.
 

Mbona hukurudi tena kuendelea na maelezo kama ulivyoahidi? tafadhali naomba urudi kama ulivyoahidi kwani hata mimi nina haja ya kutaka kufahamu zaidi kuhusu hii biashara ilivyo,au kama vipi tafadhali ni pm ndugu,Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…