Naomba kujuzwa kampuni bora ya Bima ya Afya

Naomba kujuzwa kampuni bora ya Bima ya Afya

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Heshima kwenu wadau wa jukwaa.

Ndugu yangu ana ugonjwa inasemekana wa neva. Ni kampun gan bora kwa bima ili kukabiliana na tiba bora nchini? Maana hii kupimwa pimwa tu bila tiba inatupiga sana pesa!

Sio mtumishi.
 
Kuna mambo mengi ya kuhusisha kabla ya kuamua ni bima ipi ujisajili nayo, hii inatokana na kama wewe ni mtu wa mjini au unakuwa pia muda mwingi pembeni mwa nchi (peripheral).

Kwangu ni vizuri kuwazia:
1: Mtandao mzuri (bima imetawanyika/kitoa huduma kwa kiasi gani hapa nchini).

2: Uimara(uwezo wa kufanya malipo ya gharama kubwa).

3: Exceptions/Limitations chache(mipaka katika matumizi).

1: NHIF Bima kubwa ina yote hapo juu.
2: NHIF Bima ndogo ina namba 3 zaidi hapo juu pamoja na kuwa na 1 na 2.
3: Strategy/Jubilee (kubwa) zina 2 na 3 , ila hazina 1 hapo juu.
 
Mtandao sikuelewa. Si unafuata huduma ilipo? Nilitaka kujua namna ya kuchagua bima inayocover tatzo husika.
 
Mtandao sikuelewa. Si unafuata huduma ilipo? Nilitaka kujua namna ya kuchagua bima inayocover tatzo husika.

Mtandao/kutawanyika kwa sehemu ambayo bima inatoa huduma zake:
Ukiumwa wakati uko Tarime/ Kigoma/Rukwa/ wilayani huduma zinapatikana kwa bima hiyo?
Au bima inakatwa kwa tatizo husika tu?

Kuhusu ku-cover, bima namba 1 na 3 zinacover pia ukienda kwa wahusika huwa wanatoa maelezo specific.

ILA, ukienda kama mgonjwa na gharama pia huwa ni changamoto pia/ gharama huwa kubwa zaidi kufungua bima, wengine wana muda wa ku-mature ili uweze kupata huduma za hela nyingi.

Piga huduma kwa wateja kwa bima husika ongea nao wakutumie taratibu, limitations na uone wapi panakufaa kulingana na vitita vyao.
 
Mkuu tunaomba utumie lugha rahisi na rafiki tufaidike wengi.Japo umeandika kiswahili ndani kina ugumu flani.
 
Back
Top Bottom