Naomba kujuzwa kazi ya button hii kwenye gari yangu

Inabadilisha shabaha ya taa zako kwenda juu na chini.

Ukipakia mzigo mzito kwenye gari, bila shaka upande wa nyuma unalala na upande wa mbele kunyanyuka. Jambo hilo linasababisha taa zako kupiga juu na hivyo kuumiza madereva wa magari unayopishana nayo.

Hivyo basi ukijaza mzigo/watu unatakiwa ushushe shabaha ya taa zako zipige chini kabisa kuzuia hilo, na wakati gari ikiwa haina mzigo uzilengeshe juu kwa uono mzuri.
 

hapo mwishoni umesema wakati gari haina mzigo shabaha za taa uzilengeshe juu naona kama bado utawaumiza macho madereva wengine unaopishana nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…