Naomba kujuzwa kuhusu Audi A3

jaman naomba ushauri kuna gari aina ya AUDI A3 ya mwaka 2010. natarajia kuimiliki nimeipenda sana lakini nataka nijue je ni gari ambazo hazina matatizo? na je spea zake zinapatikana kiurahisi? msaada wataalam wa magar
Gari imara spare ni durable ila zingatia service
 
Nianze kwa kusema gari za kijerumani sio kama Toyota. Kabla ya kuendelea mbele labda niulize, hii itakuwa ndio gari kauka nikuvae au unalo gari lingine nyumbani?
Kama ndio gari pekee basi sio rafiki sana kwako. kwa maana pamoja na dunia kuwa kijiji upatikanaji wake wa spare sio rahisi sana. Kuna muda utakaa hata wiki 3 kungoja baadhi ya spare parts kuwasili pale ambapo hazipatikani Tanzania na Nairobi (huko ndio nearest option). Kwa kipindi hicho kama ni spare critical lazima gari ulipaki kwa muda huo hadi vipuri kuwasili.

Magari mengi ya kijerumani (VW, BMW, Audi Benz n.k) yapo very computerized (yamehama kutoka testing za kina fundi Jafari za kuchokonoa; ukianza kulichokonoa tu lazima ulipaki)

Hii ni tofauti kidogo na Toyota ambayo kidogo zinavumilia kuchokonoa (mie sio team Toyota ila najua gari zingine za Kijapan kama Nissan, Honda, Subaru, Mitsubishi na Mazda pia hazitaki kuchokonoa)

Kwa hiyo kwa kuangalia upande wa maintanance spare zake sio rahisi kupatikana muda wote na zaidi ya yote ni ghali. Sambamba na spare, mafundi wa magari ya Ulaya na Marekani ni wachache, hii ni changamoto nyingine inayoambata na spare.

Ila ni gari nzuri, very stable barabarani, mbio ndio kwake, sio za kuharibika mara kwa mara.

Kwa hayo nakuachia ufanye maamuzi na kama utakuwa na hoja nyingine nakukaribisha.
 
nashkuru sana sana kwa ushauri.. ndugu ubarikiwe
 
Nunua liwe la kwako Tu kuja kuliuza kasheshe kipindi cha mvua utaona kila Aina ya taa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kama unaishi barabara za vumbi
 
atapigwa pasi na madaladala au atabamiza tuta apasue oil sample, usimdanganye mwenzio wewe...

mbio ndio mwake, mbio unaenda mbio barabara gani, Kilwa Road ya Mtoni Kwa Azizi Ally ?
Nimepasua sump pan wiki iliopita njia ya kutoka veta kwenda mgulani jkt. Kuna shimo pale karibu na gbp nililiingia nikasikia kishindo nikajua kimeumana. Majibu niliyapata asubuhi nyumbani.
 
Nimepasua sump pan wiki iliopita njia ya kutoka veta kwenda mgulani jkt. Kuna shimo pale karibu na gbp nililiingia nikasikia kishindo nikajua kimeumana. Majibu niliyapata asubuhi nyumbani.
napajua, pabaya kinyama, VETA kwenda Mgulani JKT, mashimo yapo Chang'ombe Road inapokutana na Taifa Road mbele ya sheli... kuna maandaki ya kufa mtu

lazima upasue pan ukiwa na gari ya chini, wanaotakiwa kukatabati hiyo barabara wanapita na V8 VX, they don't feel it...Hela za kujengea wamepeleka kujenga ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma... billions of money, they don't give a poop about us..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…