Naomba kujuzwa kuhusu fao la kujitoa nssf.

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
801
Wanajf, saluti kwenu!

Tafadhari naomba kujuzwa kwa anayefahamu kuhusu ishu hii ya fao la kujitoa nssf.

" ndugu yangu aliacha kazi sehemu (mwalimu shule ya sekondari) ili aende kusoma zaidi. Akaona ni bora atumie fao lake la kuijitoa nssf. Kwakuwa alikuwa na kadi ya uanachama kabla hajapeleka ombi la kujitoa kwa mujibu wa taratibu akaomba statement ya akaunti yake ya michango tangu aanze (miaka 2 hivi). Statement ikaonyesha balance c/f hadi tarehe ya mwisho ya kuchangia ni sh. 8,560,200/= ndipo alipopeleka barua ya kuacha kazi hivyo kuomba fao lake. Baada ya mwezi, alienda kuchukua cheki yake ambapo iliandikwa sh. 4,860,300/=. Alipo uliza ni kwanini kuna tofauti kati ya statement na malipo aliambiwa andika barua ya mapunjo. Akaandika, aliporudi tena baada ya wiki 3, akaambiwa subiri wiki 2, aliporudi tena akaambiwa aende kwa mwajili wake amjazie fomu ya michango. Alipojumlisha michango yake ikawa kama milioni 3 hivi. Hata hivyo kila akienda anaambiwa subiri, subiri tu!
Naomba kujua kwanini kuna tofauti ya kiasi kwenye statement na kile ambazho yeye alilipwa? nikamsaidia kuangalia statement yake kupitia website yao- nssf, ikaonyesha kuwa balance yake hadi anaacha kazi ni ile ile ya kwenye statement ya kwanza. Je aendelee kudai mapunjo?


Ana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…