Naomba kujuzwa kuhusu gari aina ya Nissan Juke

Chabrosy

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
2,632
Reaction score
3,150
Habari wadau,

Mimi bhana nataka ninunue iyo gari na bajeti yangu ni 18M je show room naweza nikaipata kwa bei iyo mana Crown athelet yangu nimeiuza jana 13M sasa nimeongezea hapo 5M nataka iyo Nissan Juke

Nilikujaga na uzi nilikuwa nataga BMW 3 au Crown athelet nikashauriwa nichukue Crown Athelet nikaichukua kwa mtu 12M ilikuwa ina hali nzuri sana mana jamaa alieniuzia alitembelea mwaka tuu mm akaniuzia mm na mm leo nimeiuza,sasa now nataka ninunue Show room kabisa iyo NISSAN JUKE.

Nataka nifahamu changamoto zake na uzuri wake je naweza nikapata kwa iyo 18M.

Asanteni nawasilisha karibuni wadau.

NB: NILIUZA Crown Athelete kwa sababu iko chini sana na mm mazingira niliyopo now ni bsrabara mbovu arafu rafu rood sana kwaiyo inagusa sana chini ndomana nilipendelea NISSAN JUKE mana ni ya kinyama sana niko DAR kwa ajiri ya kuitafuta iyo gari nirudi nayo mkoa,ila crown athelete ni gari poa sana unyama mno nisingeiuza...
 
Huko show room ndiko kunakopatokana mikweche ya bei mbaya. Baada ya muda mfupi inaanza kusumbua. Haswa show rooms za Wapakistani, ndio wana michezo yote michafu duniani
 
Nikisema niagize jee kwa pesa iyo naweza kupata???vipi kuhusu ushuru kodi...
Pia jaribu kutembelea supermarket πŸ›’ za Mikocheni, Masaki, Oysterbay na Mbezi Beach kwenye mbao za matangazo huwa wanatangaza magari kwa bei nzuri sana.

Hakikisha leo Ijumaa unajipatia nakala yako ya Advertising Dar utakutana nayo tu
 
Extrovert ona mwenzio anataka kununua zuma
 
Juke gari nzuri sana na nadra sana kuikuta gerage..
Uzuri engine ndogo na inatembea haswaa plus iko juu
 
Ukibadirisha mawazo njoo nikupe dualis ya 2010 [emoji4]
 
Jaribu kupita Jan Japan hapo Namanga unaweza ukapata. Hao Wajapan ndio show room pekee ambayo huleta magari mazuri kwa bei poa
Mtoa mada zingatia ushauri huu nenda pale namanga msasani utapata kila Aina ya gari na bei nafuu hiyo milioni 18 ni inatosha kabisaa .
 
Vp kaka ulivuta juke?
Tunaomba mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…