Naomba kujuzwa kuhusu kupalilia Mahindi kwa kutumia viuatilifu

Asante kwa ushauri wako. Je, hii MERAXONE inafaa kwenye ufuta? Pia napenda kujua utatumia utaalam/ujanja gani dawa isipate mimea ya mazao na kuidhuru?!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mbeya branch

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haujamweleza anatakiwa atumie wakati gani na namna gani!

Sent using Jamii Forums mobile app
Changanya ml 100 Hadi ml 150,kwenye Bomba moja la mgongoni la Lita kumi natano. Pulizia shamba, juu ya Aina zote za nyasi, dawa hiyo huuwa nyasi zote, na huacha mahindi yakiwa salama. Kama nyasi Ni fupi tumia ml 100 tu
Mabadiliko Ni ndani ya dakika 45

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho kipimo anapiga kwenye ukubwa gani wa shamba?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi za kufyeka nafikirinzinafyeka nyasi za viwanja tu. Zinaweza kufyeka eneo ambalo halijalimwa miaka mingi kwa ajili ya kupalima??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo viwatilifu vinataka uwe na taarifa za kutosha, kuna jirani yangu alitumia kupalilia mahindi cha moto amekiona mwaka huu hataambulia kitu ekari nzima imeathirika na hizo dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri wako. Je, hii MERAXONE inafaa kwenye ufuta? Pia napenda kujua utatumia utaalam/ujanja gani dawa isipate mimea ya mazao na kuidhuru?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Ufuta labda uwe uwe kwenye hatua ya kutengeneza matunda kisha upige kwa chini sana na kwa umakini sana.

Ukikosea tu utaunguza kila kitu, kwa ufuta hushauriwi kutumia viuagugu kwasababu upo kwenye kundi la majani mapana ambayo yanaathiriwa na dawa nyingi kuanzia 2-4D mpaka Roundup.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
gunia 16 kwa eka 4!, pamoja na mbolea. Hiyo ni hasara kubwa sana. Tupatie ufafanuzi zaidi
1)seedco wana mbegu za aina mbalimbali tuambie jina la mbegu uliyopanda na je ulitumia vipimo sahihi vya kupandia?
2) Mbole ya samadi ulitumia ya namna gani, kuna ilikwisha oza kabisa, na kuna ambayo iko kama vumbi vumbi
3)Ulipata magonjwa gani na uliyashughulikiaje
4) Mvua zilikuwaje
Ushauri wa haraka
1) waone wataalamu wa kilimo walio katika eneo lako wakupe ushauri wa mbegu inayofaa kwenye eneo lako. Chagua mbegu zenye punje kubwa, hizo zenye punje ndogondogo hukomaa haraka na ni tamu lakini kujaza gunia ni kazi
2) Mbegu utakayonunua ina maelekezo ya namna ya kupanda - yafuate kwa ukamilifu
3)Tumia mbolea ya kupandia kama utakavyoshauriwa na wataalamu hasa DAP inafaa sehemu nyingi. Mbolea ya samadi itumike kwa uangalifu mkubwa maana unaweza kulazimika nyingi sana ili kupata virutubisho vinavyotakiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…