Toyota Cami aka Terios, ni gari nzuri mkuu, ila bei yake show room kubwa kidogo.
Kuna cha cc 660, 1.3L, na1.5L
Nakushauri uchukue Model mpya, ya kuanzia mwaka 2006 kama budget nzuri au chukua ileile generation ya kwanza, ila ilioandikwa nyuma Terios au Terios Kid, ni more comfortable.
Ila havina nafasi sana ndani, vimebana sana kuliko IST. Viko katika familia ya "kei" cars. (Kei cars ni familia ya vigari vidogo vidogo, regardless Manufacturers, na ndio ilipo originate Suzuki kei hivi vilivyozagaa mjini). Kwahiyo sio gari nzuri sana kwa familia, watu warefu pia hawapo comfortable seat ya nyuma.
Ukipata Toyota Rush ni version nyingine ya Cami.
Cami=Terios=Rush
Wese inanusa tu, ila safari ya mbali sikushauri. Hakana balance kwakua ni kembamba hafu kameenda juu kiaina (Physics form II mambo ya Centre of Gravity)
NB: njoo specific, kuanzia mwaka unayoitaka, FWD au 4WD, engine size, manual or auto transmission hafu tukudadavuzie.
Usiogope spare, mjini zipo kibao.
Kuhusu kuuza utauza tu, watu kibao mi nimeona wakiziulizia.