Naomba kujuzwa kuhusu Toyota ISIS

Naomba kujuzwa kuhusu Toyota ISIS

Lyagwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2013
Posts
1,639
Reaction score
903
Hongereni kwa majukumu ya kulijenga Taifa.

Naomba mwenye uzoefu na mwenye kuifahamu gari aina ya Toyota ISIS anisaidie kufahamu uzuri wake na ubaya wake pia.

Binafsi naipenda kwa muonekano wake wa nje na idadi ya siti zake, mengine niko gizani.

Msaada tafadhari ili niweze kufanya uamuzi sahihi.

Natanguliza shukrani
 
Ni gari nzuri,ila kwa mazingira tuliyokuwa nayo kila siku gari nzuri zinatoka.Shida muda ukifika wa kuuza huenda ikakutesa.Ila haina shida sababu nyingi kati ya gari za Toyota zinaingiliana vipuri.
 
Hongereni kwa majukumu ya kulijenga Taifa.

Naomba mwenye uzoefu na mwenye kuifahamu gari aina ya Toyota ISIS anisaidie kufahamu uzuri wake na ubaya wake pia.

Binafsi naipenda kwa muonekano wake wa nje na idadi ya siti zake, mengine niko gizani.

Msaada tafadhari ili niweze kufanya uamuzi sahihi.

Natanguliza shukrani
Uzuri
-Ni brand ya Toyota hivyo spare zinapatikana maana injini yake ipo kwenye magari mengine ya Toyota
-Ina cc ndogo ukilinganisha na idadi ya watu inaowabeba
-Nyingi zina vvti engine so ulaji wa mafuta ni wa kawaida
-Ni gharama rahisi kuifanyia service

Ubaya
Kuna zenye vvti-d4. engine hizi ni nzuri tu ila mafundi wa kibongo wengi hawana uelewa wa kutosha wa engine hizi hivyo zikipata shida utasumbuka kuitatua. Vilevile kuna utafiti unadai kuwa zina excessive burning ya engine oil ingawa Toyota wamekuwa wakijitetea kwenye hili.

ISIS zina ground clearance ndogo hivyo ikiwa imebeba uzito mkubwa inagusa sana chini labda uweke tyre zenye profile kubwa na labda uweke specer.

Kuna zenye bumper ambalo limeongezwa hili huchakaa mapema na kuharibu shoo ya gari hasa mbele hivyo nunua ambayo haina hilo bumper lililoongezwa.

Siti zake za row ya tatu zimejibana sana.

Hitimisho
Hayo machache ndiyo niyajuayo so linganisha mabaya na mazuri kulingana na mahitaji yako then utaamua!!
 
Ahsante sana ndg yangu kwa darasa nzuri kulingana na nilivyouliza. Hakika kazi kwangu. Ahsante
 
Hongereni kwa majukumu ya kulijenga Taifa.

Naomba mwenye uzoefu na mwenye kuifahamu gari aina ya Toyota ISIS anisaidie kufahamu uzuri wake na ubaya wake pia.

Binafsi naipenda kwa muonekano wake wa nje na idadi ya siti zake, mengine niko gizani.

Msaada tafadhari ili niweze kufanya uamuzi sahihi.

Natanguliza shukrani
Hutumika na makamanda wa Isis
 
Isis gari zuri sana, analo ndugu yangu wa karibu so huwa naliendesha mara kwa mara. Lina nafasi sana ndani kwa matumizi ya familia na lina mvuto wa body kwa nje. Muhimu ni utunzaji tu na kuzingatia service linadumu.

Ulaji wa mafuta ni perfect unapiga misele ya kutosha with ratio ya 10-12km per litre ukipata lenye vvt-i. Engine zake ni kati ya 1800-2000cc.

Pia kama utahitaji kwa sasa tunaliuza, liko njema sana model ya 2005 namba D!

Lyagwa
 
Attachments

  • IMG-20180306-WA0014.jpg
    IMG-20180306-WA0014.jpg
    82.6 KB · Views: 236
  • IMG-20180306-WA0007.jpg
    IMG-20180306-WA0007.jpg
    40.5 KB · Views: 191
  • IMG-20180306-WA0010.jpg
    IMG-20180306-WA0010.jpg
    88.2 KB · Views: 206
Isis gari zuri sana, analo ndugu yangu wa karibu so huwa naliendesha mara kwa mara. Lina nafasi sana ndani kwa matumizi ya familia na lina mvuto wa body kwa nje. Muhimu ni utunzaji tu na kuzingatia service linadumu.

Ulaji wa mafuta ni perfect unapiga misele ya kutosha with ratio ya 10-12km per litre ukipata lenye vvt-i. Engine zake ni kati ya 1800-2000cc.

Pia kama utahitaji kwa sasa tunaliuza, liko njema sana model ya 2005 namba D!

Lyagwa

Ahsante ndg kwa offer yako.
 
Back
Top Bottom