Naomba kujuzwa kuhusu upatikanaji wa Spea na ubora wa magari ya Jaguar

Naomba kujuzwa kuhusu upatikanaji wa Spea na ubora wa magari ya Jaguar

Mastermind Hero

New Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
2
Reaction score
2
Samahani wadau, najua humu kuna wataalamu wa masuala ya magari. Ka.a mada inavyojieleza hapo juu.

Nina mpango wa kununua gari ndogo "sedan" na katika pitapita zangu kweye page ya Be Forward, nimekutana na gari aina ya JAGUAR XF ya mwaka 2011 na bei yake mpaka kufika bandari ya Dar es Salaam.

Sasa katika mazungumzo ya hapa na pale na wadau wa magari mitaani, nimeambiwa kuwa nisijaribu kunujua magari hayo ya Jaguar kwani upatikanaji wa spea zake, mafundi wake na vipuri vingine ni mdogo sana na itanicost sana. Nimeambiwa spea zake ni gharama sana hazipatikani hapa Bongo.

Sasa ndugu zangu, naombeni ushauri hapa, maana wananiambia kuliko Jaguar, bora ninunue Toyota crown maana itanisumbua.
Lakini binafsi ninapenda sana hili gari la JAGUAR XF, naomba kwa mwenye uzoefu na magari haya, spea zake, gereji na mafundi wake wazuri anipe japo dokezo maana nimeshakatishwa tamaa juu ya gari hili la ndoto zangu [emoji58][emoji53][emoji53].
 
Kama gari imeweza kuja mpaka mkononi mwako basi spea zitakuja kwa mwendo huohuo.

Fanya kile roho inapenda.

YOLO.
 
Chukua chuma hicho spea za Jaguar utazipata Kariakoo kuna wahindi wanauza spea za Jaguar, Evolution Garage pia unaweza kuagiza na hapo Kenya spea za Jaguar zipo kibao. Mafundi utawapata kwenye gereji za European Car.

Jaguar usichukue iliyokuwa imetumika sana au yenye km nyingi sana. Kuna mkongo jamaa yangu alinunua used toka Japan ilikuwa imekula sana km baada ya muda ikawa inasumbua licha ya spare kule Kampala kuwa kibao.
 
Back
Top Bottom