Naomba kujuzwa kuhusu ushuru bandarini kutokea Zanzibar

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Wadau anaejua taratibu za ushuru wa bidhaa pale bandarini kama umenunua vitu zanzibar inakiwaje anijuze. Kama wanachaji kwa asilimia za bei ya bidhaa au wanakuangalia unafananaje ndio wanakuchaji.

Nataka nikafanye shopping huko naona vitu bei imekaa poa.
 
Usijiloge bora umalize hapo hapo kariakoo DSM
 
Pale hakuna kanuni aisee, mwaka 2019 nilitoa fridge Zanzibar kuleta Dar walinipiga laki 1 wakati bidhaa nimenunua laki 3 tuu
 
Ujue kuna ZRA , na TRA sasa kwa sasa ili kukwepa usumbufu kanunulie vitu Dar, sio zanzibar, maana bei utayonunua zanzibar na kodi utazopigwa afadhali ununulie Dar tu,
 
Mkuu ushuru si hua unalipiwa Dar na sio Zanzibar? na TRA ndio anahusika na mambo ya ushuru. ZRB mara nyingi huchukua hela ya soda tu.
 
Kwa kweli nahisi hapana kanuni, unatizamwa pasanality yako na vipi utakvyooweza kujipapatua tu. Nchi hii ni shida sana kwa kweli.

Sasa kama mtu ana TV yake moja unamlipishaje ushuru? Mamabo mengine ni ovyo kabisa.
 
Kama zanzibar ni Tanzania, naDar ni Tanzania.

Inakuwaje ununue vitu Ndani yaTanzania ulipie tena ushuru?
 
Hivi Tanzania kwanini kuna kodi mbili mbili na tofauti
 
Wadau anaejua taratibu za ushuru wa bidhaa pale bandarini kama umenunua vitu zanzibar inakiwaje anijuze. Kama wanachaji kwa asilimia za bei ya bidhaa au wanakuangalia unafananaje ndio wanakuchaji.

Nataka nikafanye shopping huko naona vitu bei imekaa poa.

Ushuru ni kulingana na gharama ya mzigo ulionao(gharama ya ulivyonunua)
 
Back
Top Bottom