Naomba kujuzwa: Kwanini hukumu katika mahakama zinatolewa kwa Kiingereza tu?

Fisi wa Dar

Member
Joined
Apr 2, 2018
Posts
69
Reaction score
52
Nimejaribu kudadisi wanaonijibu wanasema hawajui, hebu wenye weledi na vitu hivi mnisaidie!
 
Kizungu hiki.
We acha tu!
Mbele ya pilato nikahukumiwa kwa kiingereza. Sikusikia vizuri, nikahisi kama amesema nimehukumiwa jela mwaka mmoja. Nusu nidondoke na kuzimia. Kumuuliza msaidizi wake akasema kuwa nimehukumiwa kwa kuwekwa chini ya uangalizi mwaka mmoja na sitakiwi kutenda kosa kama lile.
Hii ilitokea baada ya dereva wangu kusababisha ajali ya gari na mie sikuwa nimezingatia kama ana nyaraka muhimu ikiwepo leseni inayoendana na daraja la gari alilokuwa analiendesha.
 
Pole sana mkuu. Ilikuwa mahakama ya ngazi gani?
 
Sheria inataka hivyo lakini siyo zote kuanzia Mahakama ya Wilaya kwenda juu
OK. Nisaidie ultimate reason behind. Yaani unadhani kwanini sheria iliona umuhimu wa Ngeli badala ya Kiswahili?
 
Zinaandikwa kwa sababu ya 'urahisi wa tafsiri'. Ukisoma nyaraka za kisheria kwa lugha ya kiswahili zinaleta shida katika tafsiri (interpretation). Kuondoa ambiguity kiingereza kinatumika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…