Ugali wa dona unakuwa mzuri ukiuchanganya na unga wa muhogo(udaga)... Usipike mgumu na wala usiwe mlaini sana,kooni unapita bila vurugu pia ni lishe moja wapo yenye kupendeza zaidi!.
Unaendana na mboga takribani zote iwe nyama fresh,iwe maharage bomba,mboga za majani ukikuta imewekwa na karanga unaweza jilamba kisogo! Samaki ndo hadi chozi linataka kunitoka kabisa!.
Faida nyengine ya dona halikai sana tumboni, Wala sembe wanatabu sana haswa ukikuta mtu hanywagi na maji kinyesi kinakuwa kigumu ndio maana wanaugua na bawasiri!, hawana uhakika wa kupata kila siku choo! Hiki ni kitu mbovu mbaya kwa afya ya mwanadamu aliekamili!.
Mwisho niwahase watanzania wenzangu tupunguze Sana matumizi ya vyakula vya wanga,heri kwa ambae anafanya kazi za nguvu wale wa kukaa tu mtaota vitambi Kama mnakulaga rambirambi..!