Kama ni kuweka copyright kwenye account yako ya YouTube ni rahisi sana.
Ingia kwenye dashboard ya channel yako bonyeza kwenye option upande wa juu kushoto zitatokea option nyingi kama Videos, analytics, settings na mambo mengine ukisoma utaona sehemu pameandikwa copyright hapo utabonyesha na utaletewa video zako zote ulizo upload.
Video hizo zimepangiliwa kulingana na iliyo ya karibuni zaidi kupandishwa (upload), baada ya hapo chagua video husika kisha maliza.
YouTube watakupa muda ili kuipitia kazi hiyo kujua kama ni yako kabisa na haijawahi kupachikwa kabla yako. Baada ya kujiridhisha YouTube watakutumia ujumbe kama ipo tayari kwa ajili ya copyright au imeshindwa.
Endapo ikikubaliwa watakupa option tena je, ni maeneo gani video isichezwe endapo mtu aki upload au ikiuploadiwa na mwingine je, icheze na mapato uvune wewe una yaani option zitatokea nyingi kinacho baki ni uchaguzi wako tu na kuwasilisha uchaguzi wako.