Binadamu Mtakatifu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2021
- 4,226
- 8,879
Nakushauri fika ofisi za COSOTA kama uko Dar au Dodoma.Wakuu vipi nimekuwa nikitengeneza video zangu kwenye pc sasa nataka kuweka youtube je nitapataje copyright ili kuzuia watu kucopy na kupaste.
Ukinijuza fanya mimi ni kama mwenye 0 yani sina ujuzi wowote kuhusu copyright kwa anayejua tafadhali sana nijulishe ahsante
ahsante kiongoziNakushauri fika ofisi za COSOTA kama uko Dar au Dodoma.
Kama uko Dar fika Jengo la Utumishi Kivukoni, kama uko Dodoma tembelea ofisi ziko jengo la PSSF. Utapewa maelekezo na kuhudumiwa kwa usahihi.
Achana na vishoka, watakula hela zako na kukusababishia usumbufu usio wa lazima
Ahasnte sana ngoja nijaribu hiloKama ni kuweka copyright kwenye account yako ya YouTube ni rahisi sana.
Ingia kwenye dashboard ya channel yako bonyeza kwenye option upande wa juu kushoto zitatokea option nyingi kama Videos, analytics, settings na mambo mengine ukisoma utaona sehemu pameandikwa copyright hapo utabonyesha na utaletewa video zako zote ulizo upload.
Video hizo zimepangiliwa kulingana na iliyo ya karibuni zaidi kupandishwa (upload), baada ya hapo chagua video husika kisha maliza.
YouTube watakupa muda ili kuipitia kazi hiyo kujua kama ni yako kabisa na haijawahi kupachikwa kabla yako. Baada ya kujiridhisha YouTube watakutumia ujumbe kama ipo tayari kwa ajili ya copyright au imeshindwa.
Endapo ikikubaliwa watakupa option tena je, ni maeneo gani video isichezwe endapo mtu aki upload au ikiuploadiwa na mwingine je, icheze na mapato uvune wewe una yaani option zitatokea nyingi kinacho baki ni uchaguzi wako tu na kuwasilisha uchaguzi wako.
Elimu safiMkuu katika kusajili hiyo kazi yako itabidi ufuate hatua zifuatazo:-
Hatua ya kwanza ni kupeleka maombi ya kusajili hiyo hakimiliki katika mamlaka husika ambayo ni COSOTA. Zifuatazo ni baadhi ya nakala ambazo utaambatinisha katika maombi yako.
1. Nakala 2 za hiyo kazi unayotaka kuisajili( two copies of copyrighted work)
2. Nakala mbili za picha ndogo( two passport size pictures)
3. Nakala ya kadi ya uraia(National identity card or birth certificate)
4. Mkataba unaonesha kwamba we ni moja ya wamiliki wa hiyo kazi.
Hatua ya pili ni kuyapitia hayo maombi yako kwa kina.( Examination of the copyright application)
Hatua ya tatu ni kutoa cheti cha usajili wa hakimiliki( issuance of the certificate of registration of the copyright).
Karibu PM nikufanyie kazi mkuu na utaipata kazi yako kwa muda mfupi sana.