Naomba kujuzwa namna ya kupika mtori

Naomba kujuzwa namna ya kupika mtori

The secretary

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2012
Posts
4,148
Reaction score
2,537
naomba kujuzwa namna ya kupika mtori. cc😡gfsonwin Preta
 
Last edited by a moderator:
ha haaaa, mngoni mimi natengenezaga mtori......
huo tunakunywa wangoni tu, sithubutu kumkaribisha mchaga, lol!
Ila najua vitu muhimu ni nyama/samaki, ndizi mbichi na viazi kidogo, chumvi.
1. unachemsha nyama/samaki mpaka iive.
2. unaweza hizo ndizi na viazi vinaendelea kuchemka hadi navyo viive. ubakize supu kwa ajili ya kutengenezea mtori
3. huko mijini wengine wanaweka pia caroti, hoho, nyanya........., ila si lazima
4 unatoa zile ndizi na viazi bila supu, unaweka kwenye bakuli unaponda na kijiko. zinapondeka kiurahisi sana kama hazina supu. Ingawa siku hizi watu wanatumia brenda, lol!
5. unaongeza supu kidogo kidogo huku unachanganya upate uji kwa kadiri ya uzito unaotaka. wengine wanarudisha jikoni baada ya kupata huo mtori lakini unaweza kusave baada ya kuchanganya........
huo ndo mtori wa kingoni, lol!
 
sijui nilikuwa wapi jamani sikuona huu uzi.

haya jinsi ya kupika mtori wa kimjini.
mahitaji: nyama kg 1, ndizi 6, viazi ulaya 4, karoti 1, kitunguu maji 1 chumvi kijiko kimoja na ndimu/limao moja.
Njia:
1) osha nyama tena usiikate kate kwani nyama ikipikwa bila kukatwa katwa hutoa supu nzuri zaid. iweke kwenye sufuria hakikisha sufuria yako inafunika vyema yaani amvuke usitoke hivyo ni bora ukatumia sufuria ambazo ni nzito na zenye mifunikoyake ile ya kudumbukiza.

2) kamulia limao na kisha tia chumvi. iweke maji kikombe kimoja cha nusu lita kisha funika na itenge jikoni
3) ipike nyama hadi iive iwe laini kabisa.
4) menya ndizi zako katakata vipande vidogo dogo, pamoja na karoti na kitunguu, tia kwenye nyama uliyochemsha kisha ongeza maji kidogo na endelea kuchemsha kwa moto mdogo. hakikisha ndizi na nyama zimeiva kabisa huku zikiwa na maji ya kutosha kabisa.

5) ipua chungu chako, kisha itoe nyama yako kama ilivyo, alafu chukua kipekecho pekecha hadi uwe laini kabisa hakikisha maji uliyoopolea ni yakutosha kuufanya uwe uji mzito kiasi.

tia kwenye bakuli kisha tenga mezani pamoja na nyama yako kwenye sahani.

NB: mlo huu unatosha kwa watu wazima watatu.

kumbuka mtori siku zote ni supu na supu inatokana na obuchani ukimwambia nataka nyama ya supu usinunue nyama ni nyama tu.

nakutakia mlo mwema
 
Yaani umenikumBushia Bibi yangu alivyokua anatupikia, Mmh jamani na kahali ka hewa haka halafu uwe na nyama nyingi unanogaje

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mi mtori wangu huwa naweka magimbi!
yale madogo dogo yale!
ndizi bukoba kama tano hv kulingana na idadi ya watu!
nyama kg moja(mtori si unajua ni chakula ya wachaga ,so nyama nyingi muhimu,mwanangu anasemaga mama nyama haina basi!)
kitunguu
karoti

njia
chemsah nyama iweke supu ya kutosha,angalia mimaji isiwe miiingi unaharibu ladha
menya maghimbi kisha yasugue sana kuondoa utelezi thn yakate kate madogo madogo sio sana lakini
menya ndizi na uzikate ndogondogo pia
tanguliza maghimbi kweny sufuria,kisha nyama kisha ndzi!weka supu!(usimalize supu yote yu might need some wakati wa kuchanganya)
funika,bandika jikoni.hakikisha hakuna mvuke unatoka !
wakati huo unaweza kuanda karoti na vitunguu kwa cubes ndogondogo saaana!
baada ya kama dak 20 miksa yako itakuwa bien!
thn funua weka vitunguu na karoti kisha funika tena!
ipua after 5 mns.
rudisha supu iliyobaki jikoni iendelee kuchemka!
kama mkiksa yako bado ina supu ichuje kwanza!
songa hiyo miksa ya ndizi,nyama,magimbi,vitunguu na karoti,ukiona vimekuwa ugali kabisa manake yu cna not tell ndizi i wapi na magimbi ya wapi!hapo tayari!
weka supu yako kwa uzito uutakao,(inategemea na mlaji)

hii kitu bana iliwe na chapati(kali)yani chapati ile inayochambuka i see!
uuuwih!
@cc @FP
 
ha haaaa, mngoni mimi natengenezaga mtori......
huo tunakunywa wangoni tu, sithubutu kumkaribisha mchaga, lol!
Ila najua vitu muhimu ni nyama/samaki, ndizi mbichi na viazi kidogo, chumvi.
1. unachemsha nyama/samaki mpaka iive.
2. unaweza hizo ndizi na viazi vinaendelea kuchemka hadi navyo viive. ubakize supu kwa ajili ya kutengenezea mtori
3. huko mijini wengine wanaweka pia caroti, hoho, nyanya........., ila si lazima
4 unatoa zile ndizi na viazi bila supu, unaweka kwenye bakuli unaponda na kijiko. zinapondeka kiurahisi sana kama hazina supu. Ingawa siku hizi watu wanatumia brenda, lol!
5. unaongeza supu kidogo kidogo huku unachanganya upate uji kwa kadiri ya uzito unaotaka. wengine wanarudisha jikoni baada ya kupata huo mtori lakini unaweza kusave baada ya kuchanganya........
huo ndo mtori wa kingoni, lol!
ahahahahha da mkubwa bana!
wangoni tunatishaaaje!
pana chezea kabisa sisi!
 
Best acha nikujuze kidogo mapishi ya mtori wa kikwetu

Maandalizi:
uwe na Ndizi bukoba 6pcs, viazi mviringo 3pcs nyama yeyote ile yafaa 1kg, kitunguu maji, karoti ukipenda, hoho 1pc,
na maji, mafuta ya kupikia (cholestor), chumvi kiasi, mkaa au gesi n.k.

Matarisho:

Chukua nyama yako isafishe vizuri, kisha ibandike jikoni huku ukiweka tangawizi kidogo kuleta utamu zaidi, karoti na hoho na kisha chumvi kidogo acha ichemke mpaka iive, chukua ndizi na viazi vyako osha na katakata vipande vidogo yaani kata kwa kupasua kati mapande manne kisha weka jikoni acha vichemke mpaka viive,

Ondoa nyama yako ambao imekwisha iva katakata vipande vidogo sana ili viogelee kwenye mtori wako, kisha chukua ndizi na viazi viponde au saga kwenye brenda, kisha chukua ile supu ya nyama changanya kwenye huo mkologo koroga kwa dk5 kisha weka vipande vya nyama koroga na weka chumvi kidogo kisha weka jikoni vichemke kiasi kwa muda wa dk5 au 10 kisha ongeza maji kidogo ili kuleta ladha kidogo na endelea kukologa kiasi huku ukiacha vichemke,
sasa mtori wako tayari andaa na anza kula au kunywa waweza kunywa na mkate laini sana, au chochote kile
sijui hapo utakuwa umenielewa best nakutakia mapishi mema
 
thanks sana wakuu maana nimeumiss balaa huu mtori na utumbo..
 
Back
Top Bottom