Naomba kujuzwa nauli ya kutoka Dar mpaka Mtwara

mwalimu wenu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
203
Reaction score
19
Mi ni mwalimu mpya nmepangiwa Mtwara vijijini,naomba mwenye ufahamu ya bei ya nauli kutoka Dar to Mtwara.
 
Dar Mtwara ni sh 22,000/- Mtwara Newala ni 15000 labda useme unaenda kijiji gani.
 
Makao makuu ya mtwara vijijini yapo wapi jamani.Vipi mazingira ya huko kwa ujumla.
 
Makao makuu ya mtwara vijijini yapo wapi jamani.Vipi mazingira ya huko kwa ujumla.

Mtwara ina maani hizi: Mkoa unaopatikana Kusini-Mashariki ya Tanzania
Pili: Mji mkuu wa mkoa wa Mtwara.
Tatu: Wilaya za kiutawala, ambapo kuna Manispaa iitwayo Manispaa ya Mtwara Mikindani na ndiyo mji mkuu au makao makuu ya mkoa. Ndani yake kuna Halmashauri ya Mtwara na hiyo ndiyo huitwa Makao makuu ya Mtwara vijijini. Hivyo Makao makuu ya Mtwara Vijijini kwa maana ya ofisi za wilaya zipo hapo hapo Mtwara mjini, isipokuwa shughuki zake nyingi ziko nje ya Mji wa Mtwara kwa maana ni vijijini. Diameter ya Mtwara mjini hadi mwisho mwa vijijini ni kati ya kilometa 30-85 hivi, hapo Mtwara vijijini inaisha na unaweza ukawa unaingia Lindi vijijini, Tandahimba au Masasi. Hivyo kutoka Mtwara Mjini hadi vijijin haizidi kilometa 90, tayari unakuwa umevuka vijijini na kuingia wilaya zingine nilizokuyajia.
 
Kwa Presicion Air? Kwa Fast Jet? Kwa ATCL? Kwa Chopa la Mtei & Co? Kwa Meli? Kwa Ungo?

Fafanua Mwalimu!
 
Mtwara to dar haizid shilingi 25000 , halafu wale wanaotaka kwenda newala nauli ni shilingi 25000 kwa mabasi ya Mahuta express, akida na nauli ya mtwara to Newala ni shilingi 6000 tu nawashauri kua mkoa wa mtwara kwa usafiri ni rahisi kwa mfano ukienda stendi ya mbagala rangitatu pale utapata magari ya Dar to newala moja kwa moja, kuna magari ya Dar to Masasi moja kwa moja afu kuna magari ya Dar to Tandahimba moja kwa moja hvo hauna haja ya kwenda hadi mtwara mjini
 
karibu mwl. mi nipo mtw vjjn muda mrefu tu ila kuna vjj ukipangwa huku ujiandae kisaikolojia mana....lakn ucjali me ntakua mwenyeji wako nikuonyeshe sehm nzuri wanazouza mnaz tupunguze stress....
 
Mtwara - Newala haifiki 10000, nipo Mtwara na nmeenda Newala karbun
 

Arovera tunaomba ufafanuzi zaidi kwani kuna mwenzangu anasafiri kesho kutoka dar kwenda tandahimba. Alikuwa apitie mtwara mjini ila kutokana na maelezo yako kuna uwezekano wa kwenda bila kupita mtwara mjini. Unaweza ukanitajia mabasi mazuri kutoka hapo mbagala rangitatu ili kuepuka usumbufu wa wakata tiketi? Msaada wako tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…