Naomba kujuzwa tofauti kati ya medical doctor, assistance medical officer, clinical officer na physician

Fisi wa Dar

Member
Joined
Apr 2, 2018
Posts
69
Reaction score
52
Mara nyingi hizo titles zinanichanganya. Naomba wenye weledi na mambo hayo watusaidie hasa MAJUKUMU na ELIMU zao.
 
Mara nyingi hizo titles zinanichanganya. Naomba wenye weledi na mambo hayo watusaidie hasa MAJUKUMU na ELIMU zao.
Physician ni medical doctor aliye-specialize kwenye internal medicine( mwenye masters ya internal medicine), medical doctor ni daktari mwenye degree (bachelor of medicine), Assistance Medical Officer(A.M.O) ni clinical officer aliyeongeza elimu ya medicine kwa miaka miwili. Na clinical officer ni MTU mwenye diploma ya medicine( diploma in clinical medicine)

Sasa inapokuja kwenye kazi zao ni kama ifuatavyo;
Clinical officer - huyu anaandaliwa kufanya kazi katika ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya. Ila kutokana na upungufu wa madaktari ushishangae ukimkuta hata hospitali za mikoa
Assistant Medical Officer- Hawa wanaanzia level ya vituo vya afya na kuendelea na Mara nyingi kazi zao ni kufanya operations ( surgery) ndogo ndogo, hususani za mambo ya uzazi kwa akinamama. Ila kutokana na kujifunza pamoja na on job training hawa siku hizi wanafanya hadi operations ambazo zinafanywa na ma-specialists

Medical Doctor- hawa wana bachelor za medicine kwa hiyo Mara nyingi wanafanya kazi kuanzia level ya hospital za wilaya na kuendelea. Ila usishangae ukimkuta kwenye kituo cha afya kwani wanaweza kupangiwa kulingana na uwezo wa kituo kutoa Huduma ambazo zinahitajika kuyolewa na Medical Doctor

Mwisho Physician huyu ni medical doctor aliye-specialize internal medicine. Majukumu yake makubwa ni kudeal na medical cases hususani internal medicine.

kwa kifupi hapo ni kwa mujibu wa uelewa wangu ila. Licha ya kila mmoja wapo kuwa na maeneo( level ya kituo cha kufanyia kazi) kutokana na elimu Yake kwa siku hizi kutokana na mabadiliko mbalimbali usishangae kumkuta hata physician kwenye private dispensary ambayo ni special clinic kwa internal medicine cases
 
Nakushukuru sana ndugu
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi nina swali nini tofauti ya vituo vya afya Na hospital ya wilaya kama ukivipanga kwa ngazi itapendeza kiongozi mfano zakhem pale nizahanati au kituo cha afya?
 
DMO ni District Medical Officer, huyu anakuwa ni msimamizi( mganga mkuu wa wilaya) wa shughuli za wilaya zinazohusu afya, wilayani kuna hospitali ya wilaya ambazo ndio kubwa na inasimamia vituo vya afya na zahanati zote za wilaya.
Zamani waganga wakuu wa wilaya walikuwa Assistant Medical Officers ila sasa hivi DMO wengi ni Medical Officers, na wanafanya kazi nyingi za kiutawala na kuratibu shughuli zote za afya za wilaya
WHAT ABOUT D.M.O
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi nina swali nini tofauti ya vituo vya afya Na hospital ya wilaya kama ukivipanga kwa ngazi itapendeza kiongozi mfano zakhem pale nizahanati au kituo cha afya?
Nitajaribu kujibu swali lako kama ifuatavyo:

Tukianzia level ya chini kuna Zahanati/ Dispensary.
Inafuata level ya Kituo cha Afya/ Health Center
Inafuata hospitali ya Wilaya/ District Hospital
Hospitali ya Mkoa/ Regional Referral Hospital
Hospitali ya Kanda eg KCMC
Hospitali ya Taifa eg Muhimbili National Hospital.

Natumaini hapo utakukuwa umepata kitu.
 
Swali limefanya wengi waelewe mambo haya zaidi
 
Jamaani AMO ni mtu aliyesoma na kuwa na ADVANCED DIPLOMA IN MEDICINE. achana na blaa blaa kuwa ni Clinical Officer , vikaenda vikarudi ,hivi nikiwa na Certificate ,niajiendeleza nitakawa na Diploma au Degree. Recognition yangu inakuwaje ,ni ile ile ya certificate au ile niliyonayo sasa . Otherwise sisi sote ni madarasa la 7
AMO ni Advanced Diploma holder
MD ni Degree holder na baada ya hapo huyu akijiendeleza ndipo naye hupata hadi MMed uspeshalist
 
Ni
Nimekupata kiongozi asante
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi nina swali nini tofauti ya vituo vya afya Na hospital ya wilaya kama ukivipanga kwa ngazi itapendeza kiongozi mfano zakhem pale nizahanati au kituo cha afya?
Kuna level za hospital zetu kulingana na mazingira na upatikanaji wa huduma za afya ambazo zimepangwa kulingana na huduma zinazotolewa mahali hapo na hizi hufanyiwa ukaguzi kila mwaka na inapoonekana imekidhi vigezo flani na basi hupandishwa daraja kulingana na idadi ya watu/wagonjwa pamoja na huduma na madaktari level hizo ni
1. Dispensary/zahanati
2. Health centres/vituo vya afya
3. District hospital/ hospital za wilaya
4. Reginal refferal hospital/hospital za rufaa za mikoa hizi zilikua za manispaa zamani
5. Refferal hospital mfano muhimbili mbeya n.k kwa serikali
Kila level ina vigezo vyake ni maelezo mengi ila tambua tuna hizo level kwa sasa
 
mi nazungumzia ukimaliza ordinary diploma unaenda advanced medical officer najua AMO ni miaka 2 ukiwa na experience ya miaka 3 sasa ukimaliza iyo koz degree miaka mingap?
 
mi nazungumzia ukimaliza ordinary diploma unaenda advanced medical officer najua AMO ni miaka 2 ukiwa na experience ya miaka 3 sasa ukimaliza iyo koz degree miaka mingap?
Ukiwa AMO,kwa set up ya TZ utasoma miaka 5 kupata shahada ya udaktari.
 
Certificate ya utabibu =Clinical Officer
Diploma ya utabibu= AMO
Degree ya utabibu= MD
Umekusudia kudanganya au na wewe hujui ulichokiandika?!
Clinical Assistant Officer (CAO)= Certificate
Clinical Officer (CO)= Diploma
Assistant Medical Officer (AMO)= Advanced Diploma/Higher Diploma
Medical Officer(MO)= 1st Degree
Specialist Doctor = Master of Medicine (Mmed)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…