Kwa sasa barabara sio issue sana , sema hapo issue yako ni reliability ya chombo chenyewe, kutokana na ratiba zako .ie mara 3 kwa wiki fully loaded, hujakuwa specific sana ila nitafanya assuption gari ni kipisi hivyo huvuti trailer.
Ni kwamba 93m na p 94 ni basically kitu kimoja yani zote ni 9000 cc, isipokuwa 94 ni series 4, kwa hiyo kuna mabadiliko kama ,hp katika baadhi ya 94 (210-310 hp), na cabin design .93 ni series 3 . kitaalamu hushauriwi sana kutumia engine ndogo (93 &94 )kwenye mizigo ya kwenda umbali mrefu, unless hiyo gari iwe ilikuwa special kutoka kiwandani. kama ukifuatilia vizuri utaona kuna herufi baada ya hizo namba series 3 walitumia H,-heavy duty , series 4 wametumia L, -long haulage. so kama utafanikiwa kupata 93H au 94L . zinaweza zikafaa kwa kazi zako. 93 m -medium duty ,94d -disribution hazitaadumu kwa safari hiyo unazosema....