Naomba kujuzwa tofauti za injini katika Toyota HAarrier (4WD vs 2WD)

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
784
Reaction score
327
Habari wataalamu,

Naomba mwenye ufahamu anisaidie kutofautisha hizi engine mbili za Harrier ili nifanye maamuzi yaliyo sahihi.

ACU35 - hii ni engine ya 4wheel drive. Nachohitaji kujua ni vitu viwili tu;

i. Je hii gari inazungusha tairi zote nne kila wakati au ina sensors ambazo zinafanya isukume diff ya nyuma pale inapokutana na utelezi wa tairi za mbele? Na kama ndio ina sensor, je dereva ana option ya ku'disable hio sensor ili gari isukume mbele pekee?

ii. Vipi ulaji wake wa mafuta ukifananisha na engine ya 2WD (ACU30)? Kama hii ya 4WD inakula zaidi mafuta ni kwanini au nini kinatofauisha hizi engine mbili wakati gani inatembea?

Kwa SUV ya Nissan nazielewa sana sababu ikiwa na 4WD basi lazima utakutana na button ambayo itakufanya utumie Four wheel pale unapohitaji kuitumia tu.

Nitashukuru sana kupata huu ufafanuzi.
 
nikitumia mfano wa 1MZ-FE ENGINE inayofungwa kwenye harrier/lexus rx300 ya AWD tyre huwa zinazunguka zote 4 kwa wakati mmoja. Kama nimekosea basi ni ruksa kusahihishwa. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wataalamu,

Naomba mwenye ufahamu anisaidie kutofautisha hizi engine mbili za Harrier ili nifanye maamuzi yaliyo sahihi.

ACU35 - hii ni engine ya 4wheel drive. Nachohitaji kujua ni vitu viwili tu;

i. Je hii gari inazungusha tairi zote nne kila wakati au ina sensors ambazo zinafanya isukume diff ya nyuma pale inapokutana na utelezi wa tairi za mbele? Na kama ndio ina sensor, je dereva ana option ya ku'disable hio sensor ili gari isukume mbele pekee?

ii. Vipi ulaji wake wa mafuta ukifananisha na engine ya 2WD (ACU30)? Kama hii ya 4WD inakula zaidi mafuta ni kwanini au nini kinatofauisha hizi engine mbili wakati gani inatembea?

Kwa SUV ya Nissan nazielewa sana sababu ikiwa na 4WD basi lazima utakutana na button ambayo itakufanya utumie Four wheel pale unapohitaji kuitumia tu.

Nitashukuru sana kupata huu ufafanuzi.
Kitu cha kwanza. ACU30/35 ni Model/chasis number na sio engine number. Hizi engine zake zote ni 2AZ FE.

Kitu cha pili,, hizi ACU 35 ni full time four wheel drive kwa hiyo hakuna option ya kudisable kama ilivyo kwa nissan. Hivyo ukiinunua ujue muda wote upo na 4WD. Na ulaji wake wa mafuta ni mkubwa kuliko hizi ACU 30.

Ila kibongobongo usipokuwa makini utaina bei ya ACU 35 ipo chini kuliko ACU30 na engine ni moja ukakimbilia,,wese lake sasa.

Karibu.

Asante kwa huo ufafanuzi, yes nlisahau kuweka engine type hapo, the famous 2az ambayo ipo kwenye gari nyingi tofuaut za Toyota.

Kingine nachopenda kujua, je hii AWD kwa barabara zetu zilizojaa mchanga, matope na utelezi zinasaidia kweli?
Sina shida na Nissan, ukibonyeza button ya lock diff haukwami sehemu inakua na nguvu sana.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Yes inasaidia na ndio lengo lake haswaa. Ila ujue pia hizi nyingine ACU 30 zina namna yake ya kupambana na changamoto kama hizo,, kama Traction control nk. Hivyo basi hakuna tofauti kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes inasaidia na ndio lengo lake haswaa. Ila ujue pia hizi nyingine ACU 30 zina namna yake ya kupambana na changamoto kama hizo,, kama Traction control nk. Hivyo basi hakuna tofauti kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa uelewa huo. Siku zote nlikua naamini SUV za Nissan ndio reliable zaidi off-road na kwenye barabara za kukwama. Kumbe hata hizi za Toyota ambazo ni AWD zinasaidia pia ingawa kwenye wese kuna utofauti kidogo

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa uelewa huo. Siku zote nlikua naamini SUV za Nissan ndio reliable zaidi off-road na kwenye barabara za kukwama. Kumbe hata hizi za Toyota ambazo ni AWD zinasaidia pia ingawa kwenye wese kuna utofauti kidogo

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Kumbuka pia driving skills za dereva ni muhimu mno. Kama hina hata upewe nininutalaza gari maporini au matopeni,, au mtu ambaye hana 4Wheel akakuacha umenasa na gari yako yenye 4 wheel. So ni combination ya vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa uelewa huo. Siku zote nlikua naamini SUV za Nissan ndio reliable zaidi off-road na kwenye barabara za kukwama. Kumbe hata hizi za Toyota ambazo ni AWD zinasaidia pia ingawa kwenye wese kuna utofauti kidogo

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Mkuu, hizo gari zina AWD na sio 4WD. AWD lengo lake sio kwenda offroad hata kidogo. Hizo gari zinaweza kukwama kwenye tope dogo saana ukabaki unashangaa. Lengo lake hiyo AWD ni kukusaidia gari kuendesheka kwenye mazingira yenye utelezi wa kawaida, kama mvua kwenye lami au snow. Ndio maana inaengage yenyewe baada ya mifumo ya gari kugundua utelezi. So huweni ilinganisha hata na Nissan xTrail. AWD ya Subaru Forester iko vizuri saana kulinganisha na hiyo ya Harrier.
 
Hiki unachosema ndicho nlichokua nahisi lakini sina uhakika. Asante kwa ufafanuzi. Kwahio bora tu kununua 2WD kama lengo ni kutafuta SUV ya off load ya Toyota. Better option would be Prado ila pesa yake ndefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki unachosema ndicho nlichokua nahisi lakini sina uhakika. Asante kwa ufafanuzi. Kwahio bora tu kununua 2WD kama lengo ni kutafuta SUV ya off load ya Toyota. Better option would be Prado ila pesa yake ndefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu, kwa kifupi, Harrier/Lexus RX ni just a road car, haijatengenezwa kwa lengo la kwenda offroad. Iko platform moja na Toyota Camry (a salon car). Kama ulishaichunguza vizuri, utagundua hata gound clearance yake ni kidogo. Ile ni salon car imeinuliwa kidogo na kuwekewa bodi kubwa.

Vile ni front wheel drive, kwa dereva anayeijulia, ni vigumu saana kuikwamisha. As likishapita tairi la mbele, possibility ya kuchomoka la nyuma ni kubwa. Shida inaanzia pale jamaa wanapoibebesha mizigo kibao nyuma utafikiri wako kwenye Land Cruiser. Hapo lazima ititie.

Ila kama umepata ya AWD, ni sawa, maana sidhani kama kuna tofauti kubwa kwenye matumizi ya mafuta.
 
Back
Top Bottom