Naomba kujuzwa ubora wa Magari haya makubwa kiutendaji

Naomba kujuzwa ubora wa Magari haya makubwa kiutendaji

JJELIAH

New Member
Joined
Jul 16, 2024
Posts
2
Reaction score
2
Habari,

Naomba kuuliza mtalaam anejua malori aina ya Daf FX 2019 na Man TGX 2018 26,500/26.460 BLS 6×2 MIDLIFT.

Kuhusu ubora wa hizi gari kiutendaji kazi pamoja na gharama za spea zake na je zinapatikana kwa urahisi?

Nataka kuanzisha kampuni ya kusafirisha mafuta njee ya nchi. Ushauri tafadhali.

Screenshot_20250130-154955.png
Screenshot_20250130-145306.png
Screenshot_20250130-145306.png
 
Chukua Man Diesel ndio itahimili kazi zako. Pia hakikisha uwe na mafundi wawili au watatu na workshop kwa ajili ya gari zako zikirudi safari kwa ajili ya service kubwa.

Baadhi ya spare kama oil,grease,hydraulic,brake fluids,air na diesel filters nunua kwa jumla weka stoo zitakuwa zinatoka wakati wa service
 
Kwa huku Ulaya DAF zinafanya vizuri ila kwa Africa sijui
MAN pia nimeziona sana TZ
Lakini kama zinaenda nje kwanini usinunue Benz na Scania maana hizo ndio naona ziko vizuri zaidi
Nimeziendesha na zina raha yake especially Benz
Ila inategemea na mfuko wako mkuu
DAF ya 2015 unapata kwa £5500 wakati Scania ya 2015 inagharimu mpaka £15,000
Chaguo lako
 
Biashara ya kusafisha mafuta kwa sasa nunua gari ya kichina na trela la alluminium za afrika kusini.
Mitumba ya ulaya waachie wanaosafirisha mbao na mazao kusini.
 
Back
Top Bottom