Wasalam wandugu, nataka kununua gari kwa mtu ana kadi OG ila hana importation documents za hiyo gari. Nae kanunua kwa mtu bila hizo hati. Je, vitanizuia kua mmiliki halali wa hiyo gari?
Hapana haitokuzuia kuwa mmiliki halari wa hiyo gari.
Ila cha kufanya, omba kwanza copy ya hiyo kadi OG, nenda kahakiki umiliki wa hiyo gari sehemu husika, Ukikuta umiliki ni sahihi, Endelea na taratibu za manunuzi kisha badili kadi ya gari iwe katika jina lako.