Habari ya kutwa wanaharakati.
Nahitaji leseni ya biashara
naomba kujua utaratibu ukoje mpaka napata leseni.
Tin number tayari ninayo
Nenda ofisi za wilaya, uliza afisa biashara wa wilaya, watakupa fomu utajaza then watakukadiria kiwango cha mwaka kulipia lesseni, ukishalipia utaambiwa siku ya kuja kuchukua leseni yako. Document za kwenda nazo ni copy ya TIN Number, copy ya kitambulisho na copy ya mkataba wa kupanga eneo la biashara.
Mkuu si rahisi kama unavyomuelekeza kweli utaratibu ni huo ila kuna ulasimu hasa temeke, na sio hapo tu, ukifika wanakagua hizo doc'zako wanakupa form ambayo utatakiwa kuizungusha kwa afisa afya, mipango miji, polisi wote hao wakusainie, ndio ngoma inaanza au anakwambia wewe acha 200,000/ aizungushe mwenyewe!!! ukikataa anakwambia ok, we unaanzia kwenye ofisi ya afya wanakwambia lazima waje eneo la biashara wakague, uchekiwe afya au uwape laki moja, toka hapo nenda mipango miji, nako wanakusubili, kidogo polisi angau wao si sana hata 5000,una gongewa muhuri,. unakuja pata leseni umeshatoa karibia laki 3,hasa manispaa ya temeke ndio wamezidi. hata kama ni leseni ya kiosk tu mlolongo wake ndio huo, ni kitu ambacho kinapelekea mtu anakata tamaa na kuamua kufanya tu biashara bila leseni na liwalo liwe kwani nimechoka
Na mm nahitaji lakini biashara yenyewe ni ya usafirishaji mazao na mifugo, nifanye nini?mi nahitaji leseni ya biashara. lakin biashara yenyewe sio ya chakula wala vinywaji...
Mh sio kweli..mambo rahisi sana kwa sasa mimi niliprocess leseni ya biashara ya vitu vya watoto 2016 hakuna urasimu kama huo.uwe tu na doc zote hitajika.tin,mkataba wa pango,na copy ya kitambulisho.Duh.Hii nchi majanga kila sehemu,sijui nihame nchi?