Naomba kujuzwa uzuri na Ubaya wa Nissan caravan

Naomba kujuzwa uzuri na Ubaya wa Nissan caravan

Mtoto Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2014
Posts
300
Reaction score
173
Habari wana jamii!,

Ni hivi nahitaji kushare uzoefu kwa wale waliowahi au wanaotumia Nissan caravan kwa ajili ya Daladala,sababu nami nataka kuachana na Toyota kabisa!

1591174811826.png
 
Toyota ni gari bora ukilinganisha na Nissan.

Huo ndio mtizamo wangu baina ya gari mbili hizi. Zote mbili nimetumia na Toyota iko juu.

Spare za Toyota hazina usumbufu na mara nyingi kuuza Toyota ni wepesi tafauti na Nissan.
 
Tatizo la Toyota hiace spare zake ni nyingi lkn zimejaa feki unaweza kufunga leo kesho ikasikia imekufa tofauti na Nissan bila kusahau pia kwenye Toyota hiace unaweza kufanyiwa change kota kibao tofauti na Nissan
 
Hio inaenda bei gani mpaka ifike bongo, msaada hapo Coz Nina mpango wa kuvuta kipanya siku za usoni
 
NISSAN CARVAN
NEW MODEL 2013

..

Nissan Caravan kwa sasa inajulikana kama NV350 Caravan ndani ya japani Japan na Nissan Urvan wengine huita katika masoko mengine gari hii ni nzuri mno kuanzia umbo mpk nguvu ya injini ipo sana kwenye swala la nguvu Mshindani mkubwa wa nissan ni Toyota HiAce.

Katika soko toyota anauza sana haice zake kutokana na kuwa na jina kubwa na nissan anafanya kazi kubwa sana kuonyesha ulimwengu kuwa yeye ni bingwa nabukweli ni kuwa toyotabubora wake ni kwenye makaratasi tu lkn linapokuja swala la kushindanisha kiuhalisia nissan na mazda wanamtoa jasho kubwa , . Moja ya gari waliyotoa ni NV350 katika toleo hili hakika nissan wamepiga hatua kubwa mno ..

..Tafuta hii gari uombe kuendesha ndio utajua kile mm nachomaanisha ...gari hii inateknolojia ya hali ya juu sana , pamoja na kuwa toyota haice ...imetumika kwa muda mrefu ila kwa sasa nissan imepindua meza nanimeanza kupendwa sana katika model mpya za gari ndogo za abiria
Hebu tuione gari hii inakuja na vitu gani

Umbo la gari ni .Van
Extras: Cooler Box
Safety Features: 3 Point seat belts with ELR, ABS, brake assist, Driver and Passenger SRS Airbags, rearview camera, Seat belt pretensioner
Exterior Features: Alloy Rims(optional), Fog Lights(optional)
Interior Features: CD/Radio player, Tilt Steering

Hivyo ni baadhi ya vifaa vinakuja katika toleo la gari hili ya NISSAN.... Hivyo kuifanya kuwa bus dogo lilo bora sana

Katika uundaji wa gari hili wamezingatia mambo yafatayo

[emoji108] By length – Standard and Super Long
[emoji108] By width – Standard and Wide)

[emoji108] By Roof Shape – Standard and High Roof
[emoji108] By Floor Shape – Standard and Low
[emoji108] By Doors – 4 Door and 5 Door

Nissan Caravan inakuja na aina 3 engine options. Ambazo ni
[emoji91] 2.0L QR20DE Petrol engine,
[emoji91] 2.5L QR25DE petrol engine
[emoji91]2.5L YD25DDTi turbo diesel engine
Upande wa transmition

Inakuja na 5-speed automatic
na 5-speed manual transmission pia inakuja na machaguo mawili ya 2WD na 4WD

Nissan NV350 Caravan Grades

[emoji108][emoji108] Nissan Caravan DX – Toleo hili ni la kawaida linakuna na umbo la Van na Wagon versions. Katika toleo hili linakuja na key ignition, tilt steering, large capacity center console box, more legroom, bi-xenon headlights, front ventilated disc brakes na fuel consumption display hii kwenye gari za toyota hawana

[emoji108][emoji108] Nissan Caravan GX – Toleo hili ni toleo la kati linakuja na ; Auto light system, electric retractable side mirrors, intelligent key na push to start

[emoji108][emoji108] Nissan Caravan Premium GX – Toleo hili linakuja na 15-Inch alloy rims, chrome finish, fog lights, back view monitor and seat back pockets

Katika toleo jipya la nissan carvan inakuja na teknolojia inayoonyesha umbali uliotembea na kiasi cha mafuta ulichotumia kwa lita ...yaaani hadi raha kabisa ....ni bonge la gari la kisasa

Vifaa vya kiusalama katika gari hili ninpamoja na

: Driver na Passenger SRS Airbags, ABS, Brake Assist, Seat belt pretensioner, 3-point seat belts with ELR, Rearview Camera

Nissan NV350 Caravan Exterior

Nissan Caravan umbo lake lina fanana na toyota haice kufanana huku ni pamoja. Na size na umbo lakini Caravan inakuja na utofauti kidogo upande wa mbele ambalo ni kubwa na gumu sana ,katika grade ya GX na Premium GX inakuja na mambo ya ziada kama alloy rims na fog lights

Cabin Storage
Gari hii inakuja na sehemu kadhaa za kutunzia vitu mbalimbali katika sehemu hizo unaweza kutunza vitu kama smartphones, beverages, goggles, handbags etc. Inakuja na 4 cup-holders, door panel storage 2-compartment glovebox na center-box

Upande wa mafuta inatumiaje kwa kuwa nigari ya abiria utumiaji wa mafuta inakuwa ni tofauti na gari ndogo kwa kuwa inabeba uzito mkubwa

[emoji91] Nissan Caravan 2.0L petrol inatumia km: 9.9 Kwa lita 1

[emoji91] Nissan Caravan 2.5L Petrol inatumja km 9.1 Kwa lita 1

[emoji91] Nissan Caravan 2.5L Diesel inatumia km: 12.2 Kwa lita 1

2013 Nissan NV350 Caravan Acceleration

2[emoji108] Nissan Caravan 2.0L petrol accelerates inatoka 0-100km/h kwa 16.3 sec

[emoji108] Nissan Caravan 2.5L Petrol accelerates inatoka 0-100km/h kwa 15.2 sec

[emoji108] Nissan Caravan 2.5L Diesel accelerates inatoka 0-100km/h kwa 14.8 sec

GROUND CLEARENCE
Katika gari hii inakuja na uvungu wa gari ambao ni inch 6.7 inch ...inakuja na bonge la uvungu ipo tayari kwenda mjini au kijijini ....unapokuwa na NISSAN CARVAN ondoa shaka ni moja kati ya gari inayofanya vizuri zaidi hasa barabara ya off road na sehemu za milima na uhimilivu mkubwa kuliko toyota haice new model E 200

CHANGAMOTO ZA GARI HII
Kwa kuwa mpk sasa hakuna gari dunia isiyokosa changamoto ..hivyo hivyo hata kwa nissan carvan new model pia imeonyesha baadhi ya changamoto zake ,Baadhi ya changamoto zilizoripotiwa ni

[emoji108] Loss of power

[emoji108] Turbo failure

[emoji108] Transmission failure

[emoji108] Injector problems

Matatizo mengi kwa uchunguzi inaonyesha wazi yamesababishwa na watumiaji wenyewe kwa kuacha na kupuuzia manual book ya gari ..kuisoma na kufata yale yaliyoa agizwa na mtengenezaji

1.uwekaji wa mafuta machafu ..hasa yaliyochakachuliwa

2.uchelewaji wa kubadili oil kwenye injini na gia box

3.kutotumia oil sahihi inayosisitizwa katika new model hii itumike matokeo yake watu wanaweka oil za kawaida waliozoea kuweka katika toyota lazima ikuzingue tu

4.ufanyaji wa service zisizo kidhi vigezo hasa kupeleka kws mafundi nyundo

Haya ni baadhi ya makosa wamiliki wa nissan carvan new model wamefanya na yamepelekea matatizo niliyoyataja hapo juu ..nini kifanyike baada ya kuharibika unajua mwenyewe ...siongei kitu ....maana wa Tz tumezidi ujuaji mwingi ndio hayo ...sasa mnabaki kusema nissan wana gari mbovu wakati sio kweli ...huo ni uwongo na uzuzu kama hujui kitu nyamaza ...[emoji123]...fanya tafiti za kutosha ndio utoke ueleze .........nissan yoyote ukitaka uifurahie fata yale yaliyoandikwa kwenye manual book ya gari aiseee utafurahi sana

NINACHOPENDA KATIKA GARI HII
[emoji108]Nguvu ya injini ni kubwa hasa injini ya dizel

[emoji108]inakubali kupangiwa root yoyote na ikakuinhizia hela ya kutosha

[emoji108]inabeba idadi kubwa ya watu

[emoji108]Umbo lake ni imara sana

Nisichopenda katika gari

[emoji91]Injini hasa ile ya petrol inahitaji sana umakini mkubwa gari linapojaza sana 2.0L inazidiwa (under powered

[emoji91]Injini ya dizel ni nzuri ila inahitaji umakini mkubwa katika matunzo na uwekaji wa mafuta

Nini ufanye baada ya kuinunua
[emoji91]Jaribu kuiongezea ground clearence 6.7 inch isogee mpk 7.2 inch halafu
[emoji91]Zungusha bomba kwa chini ili kulinda bodi ya gari na kuiongezea uimara
[emoji91]Mbele nunua ngao maalumu kulinda shoo ya gari usiweke bomba la kuchomelea utaiongezea gari uzito
[emoji91]Usibandue vitambaa vya ndani ukifanya hivyo utakuwa imeishusha thamani gari yako

Upande wa spare
Spare za nissan zipo zimejaaa tele ni wewe tu hela yako

BEI YAKE NI NDOGO SANA UKILINGANISHA NA TOYOTA HAICE NI SHILINGI MILION 26

kuna watu wananijaribu bei nimeweka ipo wazi kuna jitu linauliza sh ngapi huko ni kunitafuta sasa nina majibu ya kukata na shoka ujinga staki ....

Mwisho
Kama unafikilia kufanya biashara ya kusafirisha watu .....bac ni vyema ukaifikiria gari hii ....itakutoa kimaso maso sana kuna root ukiipangia laziam a tu ....utoboe ....acha uwoga nissan ni gari nzuri ...kwa sasa TOYOTA wamejisahau wanaunda magari kwa kulipua hata katika forum moja kuna ENGINEER mkuu wa magari yupo chuo kikuu cha london kadhihirisha kwa kusema ni muda sasa wa dunia kws kuangaria aina nyingine za magàri kws kuws toyota wameshindwa kuwapa watu ...hitaji lao na mm nakwambia hitaji lako unaweza kulipa kwa NISSAN ...karibu ulimwengu wa nissan
Leo nimeenda deeep sana cjatumia ile lugha japo nimeimiss sana ....





sent from HUAWEI
 
Umechambua vizuri sana. Naipenda sana New Model ya Caravan, napenda sana muonekano wake na comfortability ya ndani ya gari.
 
TOYOTA
sifa zake
ni gari ngumu sana
inaimili sana mikikimikiki
spea zake vipo nyigi sana
ukipata 5L(ndama) ni nzuri waidi
kwenye special (private) zinapendwa sana kwani kwenye masafa marefu ni shida

NISSAN
hapa nazungumizia QD 3.5 NA TD 2.7( Kwa arusha xipo nyingi)
ni gari ngumu sana na ni roho ya paka TD
spea zake zipo nyingi tu
ila zinaanza kuchoka ukilinganisha na toyota
bodi yake ni laini
bei yake ni nafuu ukilinganisha na toyota
itaanza kuchoka kabla ya toyota

ushauri wangu kama unaanza biashara hii , tafuta nissan caravan TD 2.7 Kwan hii ni ngumu sana na maspea yapo ya
kutosha ila kama mfuko unaruhusu chukua TOYOTA 5L a.k.a ndama

niko tayari kukosolewa
 
Umechambua vizuri sana. Naipenda sana New Model ya Caravan, napenda sana muonekano wake na comfortability ya ndani ya gari.
shida ya hii new model kwa biashara ya daladala inaweza kuwa mtihani kwan waliokuwa nazo wanalalamika sana sasa sijajua shida ni nini ila kwenye makampuni ya utalii naona zipo(nazungumzia kwa uzoefu wa arusha)
 
shida ya hii new model kwa biashara ya daladala inaweza kuwa mtihani kwan waliokuwa nazo wanalalamika sana sasa sijajua shida ni nini ila kwenye makampuni ya utalii naona zipo(nazungumzia kwa uzoefu wa arusha)
Kwa biashara ni changamoto. Inatakiwa kutumika kama STAFF Bus au Shughuli kama hizo za utalii.
Kazini kwetu karibia staff zote ni Nissan Caravan, Hommy na Urvan.
Ziko poa sana.
Leopard tours pia wanazo za kutosha.
 
Tafuta yenye engine ya Diesel.. Manual au auto naona zote zina consumption sawa.. Iko vizuri.. Tatizo nililoliona ni bumper za plastic.. Weka ngao kuzilinda.. Zinatoka sana unyoya.. Usinunue yenye Turbo.. Dereva ataua abiria.
Kwa kipindi kifupi nilicho kuwa nayo, nilisha gombana na watu wengi sana bara barani.. Gari iko swift, so rough zinakuwaga nyingi kidogo ukikaa kwenye usukani!
 
Kwa Nissan Caravan New Model usiifanye daladala ni bora ukafanyia kazi za kuikodisha, kubebea wanafunzi au kubeba watalii.

Toyota kamwe Heshima yake Africa,Asia na America kusini haitoshuka ni gari isiyokupa mawazo.

Hiyo Nissan Caravan kwa mbilinge mbilinge za daladala utagombana na dereva.
 
Back
Top Bottom