Naomba kujuzwa uzuri wa hii Noah new shape

edger jairos

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
335
Reaction score
71
Naomba kuuliza Uzuzr wa gar hiii katika soko hasa kwa matumizi ya apa mjini


 
Kaa nayo mbali sana hiyo mkuu, usije ukashawishika kuichkua. Utakuja kujuta. Nimetoka kuiuza yangu kwa hasara sana december mwaka jana. Kama unataka Noah chukua old model bila kupepesa macho, utanishkuru baadae
Kwa hasara aje?

Mwamba uliinunua kwa 10M ukataka uiuze kwa 15M?
 
Kwa hasara aje?

Mwamba uliinunua kwa 10M ukataka uiuze kwa 15M?
Niliinunua 2015 mwishoni kabisa, lengo lilikuwa niingie mkataba na hotel flani iwe inatumika kama shuttle pale airport, hilo likafanikiwa. Baada ya muda jamaa wakanunua coaster, hivyo mkataba wa awali ulivyoisha hawakurenew tena. Goma nikabaki nalo mwenyewe kwa matumizi yangu mengine, ingawa halikua lengo. Kimbembe kilianza ilivyoanza kusumbua ishu za umeme na engine kuzima yenyewe ghafla. Pia lile body ni kama box, hamna kitu zaidi ya muonekano tu. Nilipambana nayo sana mpaka nkaamua kuiuza. Madalali wakasema uhitaji wa zile noah ni mdogo sana tofauti na old model. December 2020 nkaja kubahatika kupata mteja, nikaiuza kwa mbinde kwa 6M. Kwangu nimehesabu ni hasara nikiangalia bei niliyonunulia, nikilinganisha na uwiano wa pesa iliyoingiza wakati inafanya kazi + bei niliyoiuza + muda wa tangu nilivyoanza kulimiliki. Ningeinvest pesa ya manunuzi kwingine kwa hiyo miaka ingeweza kuzalisha vizuri tu
 
Gari ya 12m mwaka 2015 umeiuza 2020... 6m bado unaona ni hasara watu mna moyo aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…