Wakuu habarini za weekend niende Moja Kwa Moja kwenye mada tajwa naomba kujuzwa vipimo vya kutengeneza kashata yaan kuanzia karanga nusu na kuendelea kuanzia sukar na maji kias gan asanten sana na weekend njema
Kashata na maji tena mkuu!
Maji hayahusiani kabisa na utengenezaji wa kashata.
Kashata inatengenezwa kwa bidhaa tatu:
i-sukari
ii-karanga, ufuta, chicha la nazi(mojawapo)
iii-magarine au samli kwa ajili ya kupaka chombo cha kuipulia ili kashata isigandamane kwenye chombo.
Kipimo: kama karanga, ufuta ama machicha ya nazi nusu kilo, basi sukari itakuwa ni robo kilo.
Natoa mfano wa bidhaa moja tu(karanga) kwaajili ya mfano.
Utachukua karanga nusu kilo unazikaanga kwenye kikaango kwa kutumia mkaa, zikishakuwa tayari, utaziipua na kuacha zipoe.
Zikiishapoa, pukuchua zibakie safi bila maganda.
Andaa sukari robo kwenye sufuria che msha sukari hadi iyeyuke na kuwa na rangi ya hudhurungi inayofanana na asali.
Ipua chini sufuria yenye sukari iliyoyeyuka ikiwa bado ya moto, weka karanga ndani ya sufuria la sukari iliyoyeyuka, tumia mwiko changanyia kwa kuzungusha kama unavyosonga ugali mpaka mchanganyiko huo ukae sawa, ie: vipande vya karanga viwe vimezungukwa na myeyuko wa sukari.
Pakaza mafuta(margarine/samli) kwenye sahani ya kuipulia, kisha mimina mchanganyiko huo kwenye sahani hiyo.
Ukishamimina mchanganyiko kwenye sahani, muda huo huo bado wa moto, isambaze kwa kuitandaza ibakie na unene wa nusu inchi ama nchi moja na uiache ipoe kabisa.
Ikiishapoa, kata vipande utakavyoona inafaa.