Naomba kujuzwa zaidi kuhusu gari aina ya Nissani zinazotumia umeme

Chabrosy

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
2,632
Reaction score
3,150
Wana jukwaa habari,

Poleni na corona ok any way twendeni kweny point.

Katika kujichanga changa kwangu kuna gari moja nataka ninunue inaitwa NISSAN ipo kama IST flani hivi inatumia umeme ina chajishwa aitumii mafuta hii gari nimeipenda sana wakuu.

Niliiona wakati nipo Dar, Upanga kuna mtu alipaki nikaipenda kweli kidogo kidogo ivi nilikuwa nataka ninunue. Je, ni shilingi ngapi? Mimi nina 8M niko mkoa wa Njombe, Makambako.

Yeyote anayeijua hii gari vizuri na bei yake na uimara wake na ninaweza ipataje.

121.
 
Sijui Kama ndio hiyo ila hii kufika bandarini ni milion 7, andaa Kodi zingine za TRA + Bima
IMG_20200428_085036.jpeg
IMG_20200428_085109.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hi hii aisee asante sana bro kodi shi ngapi hapo.

121.
 
Mimi nikushauri ndugu yangu mwana njombe mwenzio.

Mimi ni mwangimbudzi wa hapo hapo njombe ni fundi nipo kwenye anga hizi zaidi ya 10yrs. Hebu badili wazo lako hilo tafuta au nunua aina nyingine ya gari shida ya hizo gari ni spare na spare au ugonjwa wake mkubwa ni HV battery.

Na mpaka zinauzwa huko kwao zishakuwa majanga au zinaelekea kwenye umajanga ww utatembelea hata mwaka hautoisha itakuzingua au hata miaka miwili itakuzingua na mbaya zaidi sisi huko tunaziua sababu ya washa zima washa zima. Mtu ana washa gari mwenge anakwenda mliman city anazima amefika anakaa akitoka hapo anawasha gari anakwenda ubungo amefika safari yake.. atatoka hapo analudi mwenge hivyoo yaani vijisafari vifupi fupi na huwezi iacha kwa muda mrefu utasema mafuta yanakwisha.

Hizo gari hazitaki mambo hayoo.. kingine betri ikisha kwenda down mashine za kuchaji ni changamoto kidogo ingawa zipo chache hapa mjini na ugonjwa mwingine mkubwa ni motor ya maji. kuna motor ya maji ya kupooza inverter converter hiyo mara nyingi inakufa sababu wabongo tunaweka maji au coolant ya kawaida lakini kuna maji yake special yanakuwa kama mafuta flani hivi..garama ya betri unaweza nunua kavits kangine kamkononi.
 
Aisee asante kwa ushauri bro nitautfanyia kazi

Hivi zipo sheli hapa mjini ambapo zinatoa huduma ya kuchaji gari?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom