Habari zenu wadau. Jumamosi majuzi mwanangu alilazwa hospitali kwa shida ya maleria akiwa na kilo 13. Akadungwa sindano za kwinini akawa mzima tukaruhusiwa lakini daktari akasema anywe kwinini ya vidonge nyumbani. Alivyomaliza sindano alipungua sana joto na alionesha ahueni. Sasa kwinini anachoka na analala sana. Naomba ushauri wenu tafadhali.