Naomba kupata ufahamu kuhusu utaratibu wa 'sick sheet'

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Kuna hiyo kitu kwa wafanyakazi wa serikali pale anapougua, nasikia hutolewa na halmashauri husika.

Naomba kuelewa kidogo kuwa hutolewa vipi na hujazwa muda gani. Mfanyakazi aliye likizo na kuugua huko, utaratibu wake wa matumizi ya hii upo vipi? Akirudi na cheti chake cha kawaida cha hospitali itakuwa sawa?

Ahsanteni.
 
Ukiwa Likizo ukaugua huitaji Sicksheet kwakuwa siku unazotumia kujiuguza haziingiliani na muda wa mwajiri. Inapofikia Ugonjwa umepitiliza siku za Likizo na ukaingilia siku za mwajiri lazima umwagize mtu wa karibu akujazie Sicksheet na kukutumia ili uwe nayo huko huko unakotibiwa na kila unapohudhuria Hospitali uwe nayo Daktari aijaze kisawasawa kwenye Jedwali lake juu ya tatizo linalofanya uhudhurie Hospital, vinginevyo wewe ni mtoro na Unatakiwa uchukuliwe hatua za kinidhamu. Vilevile unapaswa uwe umetibiwa hospital ya Serikali ama sivyo pawepo na rufaa ya kwenda kwenye hiyo Private Hospital. Wajuvi ongezeeni.
 
ahsante sana kiongozi kwa somo hili......umenipa mwanga haswaaa!
 
Back
Top Bottom